Kamanda Diwani Athumani. |
Mkazi wa Kata ya Ngana wilayani Kyela, Richard Mwakalukwa (23), amemuua mkewe Agnes Kalinga (18) kwa kumnyonga shingo na baadae yeye alijinyonga kwa kamba ya manila.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Diwani Athuman alitaja chanzo cha mauaji hayo kuwa ni wivu wa mapenzi.
Kamanda Athuman alisema Mwakalukwa kwa muda mrefu alikuwa akimtuhumu mkewe kutokuwa mwaminifu katika ndoa yao, kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine.
Athuman alisema mauaji hayo yalifanyika Januari 21 mwaka huu saa 9:00 alasiri, ambapo mume alimnyonga shingo mkewe mpaka kuivunja.
Baada ya kuona amemuua, akachukua kamba ya manila na kujinyonga katika mti wa mkorosho nje ya nyumba yao.
Katika tukio jingine lililotokea Januari 21 majira ya saa 12:30 jioni katika kijiji cha Hanseketwa wilayani Mbozi, gari moja liligonga pikipiki na kusababisha kifo cha dereva wa pikipiki hiyo.
Tukio hilo lilitokea katika barabara ya Mbeya/Tunduma na lilihusisha gari lenye namba T 451 BRK Toyota Coaster, lililokuwa likiendeshwa na Willy Songela, maarufu kama Muasisi (46).
Gari hilo liligonga pikipiki yenye namba T 201 CCT, aina ya T-Better na kusababisha kifo cha dereva wa pikipiki hiyo, Tito Nyondo(20), mkazi wa Tunduma.
Ajali hiyo pia ilimsababishia majeraha mwanafunzi wa shule ya sekondari, Msika Baraka Nyondo (19) ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi iliyopo mji mdogo wa Vwawa.
Kamanda Athumani alisema tukio la tatu ni la kifo cha mwanafunzi wa darasa la kwanza wa Shule ya Mwanyanje, Halaika Bushiri (7) kilichosababishwa na ajali ya moto iliyotokea nyumbani kwao Uyole jijini Mbeya.
Alisema tukio hilo lilitokea Januari 21 majira ya 7:45 za mchana wakati mtoto huyo alipokuwa amelala kwenye kochi, lililokuwa kwenye korido ulipoanzia moto, lakini baadaye ukazimwa.

No comments:
Post a Comment