KUSHOTO: Philip Morton. KULIA: Mahakama ambapo Morton alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela. |
Mwanaume anayevutiwa kufanya mapenzi na watoto ambaye aliandika taarifa za mashambulizi yake kwa msichana mwenye miaka 15 kwenye ukurasa wa kitabu chenye saini za watu maarufu aliouita "Mapenzi na Maumivu ya Moyo ya Maisha Yangu" amefungwa miaka mitano jela.
Philip Morton mwenye miaka 56, aliandika mashambulizi yake yasiyo na heshima kuhusu msichana huyo kati ya mwaka 1994 na 1995 katika kitabu, ambacho kiligunduliwa na maofisa wa polisi waliofanya msako katika nyumba yake mjini Lincolnshire.
Ndani yake Morton alieelezea jinsi alivyompatia msichana huyo zawadi za hereni ili waweze kuongea ana kwa ana wakati wa usiku, na kuandika: "Nilijikuta nikizama kimapenzi kwake... nilitumia muda mwingi tukiwa pamoja naye".
Morton pia alisema katika kitabu - ambacho hakikuchapishwa jina ila kwenye nyaraka za karatasi alizohifadhi nyumbani kwake - kwamba muathirika wake alilala kitandani kwake.
Polisi wa Humberside walisema maofisa walitumia intelijensia ambayo iliwaongoza wao kupata kibali cha kukagua nyumba ya Morton iliyoko Immingham, karibu na Grimsby, Februari mwaka huu.
Sambamba na kitabu cha kuhuzunisha, maofisa walikuta zaidi ya picha 17,000 za watoto zisizo za heshima katika kompyuta yake - ambapo takribani 100 kati ya hizo ziliangukia katika makosa ya jinai.
Mwendesha mashitaka Mark Kendall aliieleza mahakama ya Gimsby kwamba polisi walivumbua zaidi ya picha milioni kwenye mfululizo wa vitunza kumbukumbu vya kompyuta vilivyohifadhiwa kwenye nyumba ya Morton, lakini haikuwezekana kusema ni ngapi zilikuwa siyo za heshima.
Mahakama hiyo ilielezwa Morton alikuwa akitumia programu maalumu ya kompyuta kuficha baadhi ya picha, pia na taarifa za mitandao aliyotembelea na maneno aliyokuwa akiandika katika mitandao ya kutafutia vitu kwenye kompyuta.
Alipohojiwa na polisi, Morton alidai kuwa alitengeneza sehemu ya kitabu hicho na kwamba msichana huyo alimweleza ana miaka 16. Pia aliwaeleza maofisa alishavunja uhusiano huo.
Polisi walipomtafuta muathirika wake huyo ambaye sasa ni mtu mzima, aliwapa taarifa za mashambulio yasiyo ya heshima na kuwaeleza kwamba alikuwa akimwona Morton kama 'baba'.
Morton alikiri mashitaka 14 ya kumiliki picha zisizo na heshima na mashitaka mawili ya mashambulio yasiyo ya heshima kwa msichana wa miaka 15.

No comments:
Post a Comment