Mkazi wa Majengo katika mji mdogo wa Tunduma, Lega Gawa (21) anatafutwa na Polisi kwa tuhuma za kumuiba mtoto wa bosi wake na kumtelekeza kwa msamaria mwema, akidai deni la muda mrefu la ujira wake wa Sh 770,000.
Gawa anadaiwa kumuiba mtoto Lydia Itembe mwenye umri wa mwaka na miezi miwili nyumbani kwao katika Kitongoji cha Majengo, Tunduma wilayani Momba.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman alisema chanzo cha kuiba mtoto huyo ni madai ya muda mrefu ya ujira huo kutoka wazazi wa mtoto huyo, Emanuel Itembe (32) na Jane Sanga (27).
Alidai mtoto huyo aliibwa nyumbani kwao Januari 16, mwaka huu saa 1 asubuhi na Gawa, wakati wazazi wake wakiwa katika karakana yao ya kuuza mbao.
Alitumia mwanya wa kufahamu wazazi walipo na kumchukua kirahisi mtoto huyo bila wazazi kufahamu.
Alidai baada ya wizi huo, Polisi mkoani Mbeya ilianza msako kwa kushirikisha ofisi za mikoa mingine na ndipo Januari 19 mwaka huu, mtoto huyo alikutwa kijijini Dumila wilayani Kilosa akiwa hai ametelekezwa nyumbani kwa Ashura Abdulrahaman (53).
Hata hivyo, mtuhumiwa wa wizi wa mtoto huyo hajakamatwa, kwa kuwa wakati Polisi wanafika nyumbani kwa Ashura, msamaria mwema alisema mtuhumiwa baada ya kumuacha mtoto huyo hapo, aliaga kwenda dukani kununua nepi na hakupatikana tena kijijini hapo.
Kamanda Athumani alitoa wito kwa raia wema wanaofahamu aliko mtuhumiwa huyo, watoe taarifa akamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

No comments:
Post a Comment