PROFESA MANYELE ATEULIWA MKEMIA MKUU MPYA WA SERIKALI...

Dk Hussein Mwinyi.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi amemteua Profesa Victor Manyele kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.
Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Wizara ya Afya, Nsachris Mwamwaja,  ilisemauteuzi wa Profesa Manyele kushika nafasi hiyo ulianza Januari 21, mwaka huu.
Alisema, awali Profesa Manyele alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anajaza nafasi hiyo iliyokuwa wazi baada ya aliyekuwa Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Ernest Mashimba kufariki dunia Septemba 19, mwaka 2010.

No comments: