AJIFUNGIA SIKU MBILI AKIMBAKA BINTI WA MIAKA 12 CHUMBANI KWAKE...

Mahakama ya Cambridge ambako Arendse (kulia) alipatikana na hatia.
Mtu anayevutiwa na watoto kimapenzi ambaye alijibanza kwenye chumba cha binti wa miaka 12 na kufanya naye mapenzi kwa siku mbili huku wazazi wake wakiwa hawajui chochote wakiwa sehemu ya chini ya jengo hilo, amefungwa jela.
Leigh Arendse mwenye miaka 25 mkazi wa Brunswick Park, huko Barnet, alimfanyia vitendo vya kikubwa binti huyo asiye na hatia ndani ya chumba cha intaneti kabla ya kusafiri kutoka London kwenda nyumbani kwake Cambridgeshire kuonana naye.
Kisha akatumia masaa 48 katika chumba chake akitazama DVD na kufanya naye mapenzi - na kujificha nyuma ya mlango wakati mama wa binti huyo alipokwenda kumtazama mwanae.
Arendse alidai alidhani binti huyo alikuwa na miaka 14 na alikuja kugundua umri wake wa kweli wakati mama yake alipomweleza binti huyo baada ya kuhisi harufu ya sigara chumbani kwake.
Kisha akaondoka nyumbani hapo na kwenda London akiwa na binti huyo ambaye wazazi wake walitoa taarifa wakati alipotoweka Agosti mwaka jana.
Arendse, kwa sasa amefungwa miaka minne jela baada ya kukiri mashitaka mawili ya kumbaka msichana huyo.
Jaji Jonathan Haworth alimweleza Arendse: "Hii siyo kesi ya mtu wa miaka 18 au 19 - wewe ni mtu mzima mwenye akili zako.
"Ulikuwa kwenye chumba chake wakati ukijua kwamba wanafamilia wenzake walikuwamo kwenye nyumba hiyo.
"Kulikuwa na kutokuwajibika ipasavyo kwa upande wako uliposhindwa kujua umri wake halisi."
Mwendesha mashitaka Sara Walker aliieleza mahakama kuu ya Cambridge: "Mshitakiwa alikaa kwenye chumba cha muathirika ambako wawili hao walitazama DVD.
"Jioni iliyofuata, mama yake alikuja na Arendse akajificha nyuma ya mlango.
"Mama yake alimfokea na kusema kwamba binti yake hakutakiwa kuvuta sigara katika umri wake wa miaka 12. Ndipo mshitakiwa akabaini kwamba alikuwa na miaka 12."
Aliongeza: "Muathirika alisema alianza kumbusu Arendse na kwamba mwanzoni alimsukumia mbali.
"Kisha akaanza tena kumbusu na Arendse naye akambusu kabla ya kufanya mapenzi."
Mahakama hiyo ilielezwa kwamba msichana huyo aliieleza familia yake kwamba alifanya mapenzi na Arendse bila kutumia kinga.
Akitetea, David McIntosh alidai kwamba mwitikio wa Arendse baada ya kubaini umri wa kweli wa binti huyo ilikuwa moja ya 'mshituko' na aliamua kurejea London.
Alisema: "Binti huyo ndiye aliyekuwa akisisitiza kumfuata Arendse London na katika utetezi wake hakutaka kuja na msichana huyo."

No comments: