Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema. |
Wimbi la ghasia na vurugu linazidi kukithiri hususan maeneo ya Kusini mwa nchi na kuhatarisha amani na utulivu nchini.
Hali hii ikiendelea bila kudhibitiwa, huenda ikazidi kuwa mbaya na kuathiri shughuli za uchumi za wananchi.
Kinachoonekana hivi sasa ni baadhi ya wananchi kudiriki kukabiliana na vyombo vya Dola hususan Polisi, kwa kile kinachobainishwa kuwa ni kushindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo.
Ghasia za Mtwara ambazo zimejificha ndani ya suala la gesi, ni kama zinachochewa na watu wanaotaka kuuaminisha umma kwamba Serikali iliyoko madarakani imeshindwa kusadia wananchi.
Ili kuondokana na baa hili, viongozi wa mkoa wa Mtwara wanapaswa kukaa chini na wawakilishi wa kweli wa wananchi na kufikia mwafaka wa kujua nini kinahitajika na nini kifanyike.
Wakati juzi vurugu hizo zilisababisha kuchomwa kwa nyumba za viongozi wa CCM na Serikali na pia gari la Polisi, jana zilihamia Masasi ambako pia nyumba za viongozi wa CCM zilichomwa moto huku majengo ya Serikali yakiharibiwa na baadhi ya watumishi wa umma wakijeruhiwa na wengine kudaiwa kupoteza maisha.
Haya ni matukio mabaya ambayo yanaiweka nchi katika taswira hasi, ambapo kukosekana kwa majadiliano kunafanya msuguano wa chini kwa chini kuhusu malalamiko ya wakulima na polisi na wafanyabiashara wa bodaboda, vikifukuta na kuibua kadhia kama hiyo.
Habari za uhakika kutoka Masasi zilisema katika vurugu hizo, nyumba za wabunge wa CCM, Mariam Kasembe ambaye ni Mbunge wa Masasi Mjini na Anna Abdallah, mwanasiasa mkongwe ambaye kwa sasa yuko bungeni kwa tiketi ya Viti Maalumu, ziliteketezwa kwa moto.
Aidha, ofisi kuu ya CCM wilayani humo iliyopo eneo la Mkuti, nayo iliteketezwa kabla ya kundi la vijana waendesha bodaboda linalodai kuchoshwa na kunyanyaswa na askari wa doria wanaotumia pikipiki, kufanya vurugu zaidi, ikiwa ni pamoja na kuchoma jengo la ghorofa moja la Halmashauri ya Wilaya. Magari ya halmashauri nayo yaliripotiwa kuteketezwa.
Anna Abdallah, alithibitisha tukio la kuchomwa kwa nyumba yake katika eneo la Mtandi.
Kasembe ambaye hata hivyo hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, licha ya kuchomewa nyumba, alichomewa pia gari lake la ubunge aina ya Toyota Land Cruiser na trekta, ambavyo vilihifadhiwa katika nyumba yake iliyoteketezwa pia eneo la Migongo, mjini humo.
Habari zaidi zilisema, kundi la vijana hao lilivamia pia eneo la Gereza Kuu la Wilaya kwa lengo la `kuteka’ na kuwaachia huru wafungwa, lakini baada ya kudhibitiwa, lilisambaa katika maeneo mengi, ikiwa ni pamoja na Upanga iliko nyumba ya Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.
Hata hivyo, hawafanya lolote kutokana na ulinzi mkali uliowekwa, lakini walifanikiwa kufanya uharibifu katika baadhi ya nyumba, hasa zinazokaliwa au kumilikiwa na askari Polisi wa eneo hilo.
Ingawa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Maria Nzuki hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, vyanzo vyetu vilieleza kuwa, askari Polisi mmoja aliuawa huku raia takribani sita wakiripotiwa kupoteza maisha.
Aidha, ilielezwa kutokana na idadi kubwa ya majeruhi, upatikanaji wa huduma za haraka umekuwa mgumu kutokana na vurugu hizo, kusababisha kufungwa kwa hospitali binafsi tatu. Hospitali pekee iliyokuwa inafanya kazi ni Mkomaindo, ambayo ni ya wilaya.
Huduma katika soko kuu la Mkuti, maduka na migahawa na hata usafiri nazo zilikuwa adimu jana.
Hadi jana jioni, hali ilionekana kutulia kiasi, baada ya kuwasili kwa vikosi zaidi vya askari kutoka makao makuu ya mkoa, Mtwara na wilaya jirani.
Kutoka Morogoro taarifa zinasema kwamba Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Morogoro, Jacob ole Mameo, ameionya Serikali kuwa isipokuwa makini na kuchukua hatua kali vurugu zenye msingi wa kubaguana, zinazoambatana na uharibifu wa mali za watu, amani iliyopo inaweza kutoweka.
Askofu Mameo alizungumza hayo jana na gazeti hili kwa simu akiwa nje ya mkoa kuhusu kujitokeza kwa mara nyingine vurugu kati ya wafugaji na wakulima wa vijiji vya Kata ya Dumila wilaya ya Kilosa.
Alitaka Watanzania wadumishe amani bila kubaguana na kwamba Serikali isipodhibiti wachache wanaoamua kuchukua sheria mkononi na kuharibu mali za watu kwa kuzingizio cha kudai haki, Taifa litatumbukia kwenye machafuko.
Alisema, kuharibiwa kwa nyumba na mali za wafugaji wa kimasai Dumila wakati waliuziwa kihalali maeneo ya ujenzi na kuweka vitegauchumi ni dalili ya kuifanya nchi isitawalike.
1 comment:
Ѕure, in that resρect was a behemoth bang to staгt on
the motility online poκіes bandwagon -- уour giraffe іs ready!
Here is my page - online pokies austalia
Post a Comment