Askari wakihangaika kuzima moto huo. |
Takribani watu 245 wameuawa katika klabu ya usiku nchini Brazil baada ya moto kulipuka ndani ya jengo hilo mida ya alfajiri.
Taarifa za awali zilikuwa watu 90 wamekufa kwenye mlipuko wa moto, lakini askari wa vikosi vya kupambana na moto haraka wakarekebisha takwimu hizo wakati ukubwa wa moto huo ulivyobainishwa.
Jumla ya waathirika bado haijafahamika na inawezekana kuna mamia ya waliojeruhiwa, polisi jamii na msemaji wa serikali ya eneo hilo Marcelo Arigoni aliieleza Radio Gaucha.
Aliieleza redio hiyo kwamba lori lililobeba miili 70 lilikuwa limewasili kwenye kituo cha michezo cha manispaa, ambacho kimekuwa kikitumika kama sehemu ya kutambulia maiti.
Polisi wanaamini kuna takribani miili 20 bado imo ndani ya klabu hiyo.
Karibu watu 200 wamejeruhiwa, walisema.
Maofisa walisema moto ulizuka kwenye klabu ya Kiss iliyoko katika jiji la Santa Maria, kilomita 550 kutoka Porto Alegre, kusini mwa Brazil, wakati bendi ilipokuwa ikitumbuiza.
Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika, hatahivyo, Sandro Mennerz, msemaji wa polisi katika jiji la Santa Maria, alivieleza vyombo vya habari kwamba moto ulilipuka katika klabu ya Kiss wakati bendi ilipikuwa ikitumbuiza.
Gazeti la Diario de Santa Maria liliripoti kwamba moto huo ulianza majira ya Saa 8:00 usiku wa manane.
Mlinzi wa klabu hiyo, Rodrigo Moura, amenukuliwa na gazeti hilo akisema eneo hilo lina uwezo wa watu kati ya 1,000 na 2,000. Alisema watu walikuwa wakisukumana na kukanyagana wakijaribu kujiokoa.
Ezekiel Corte Real, 23, alinukuliwa na gazeti hilo akisema aliwasaidia watu kujiokoa. "Niliweza tu kutoka nje sababu nina nguvu mno," alisema.
"Jumapili ya majonzi", alituma Tarso Genro kwenye mtandao wa Twitter, gavana wa jimbo la kusini la Rio Grande dol Sul. Alisema hatua zote zinazowezekana zilikuwa zikichukuliwa na kwamba atakwenda jiji humo baadaye leo (jana).
Santa Maria, ulioko ncha ya kusini mwa Brazil karibu na mipaka ya Argentina na Uruguay, ni mji mkubwa wa chuo kikuu wenye idadi ya watu takribani 250,000.
Moto huo unaonekana kuwa miongoni mwa ya hatari zaidi duniani kutokea kwenye klabu za usiku tangu mwaka 2004 moto ulipoua watu 194 kwenye klabu iliyofurika watu mjini Buenos Aires, nchini Argentina.
Moto kwenue klabu ya Lame Horse mjini Perm, Urusi, ulilipuka Desemba 2009, pale mafataki yaliyopigwa ndani kudaka kwenye dari la plastiki, na kuua watu 152.
Moto kwenye klabu ya usiku nchini Marekani ya Rhode Island mwaka 2003 uliua watu 100 baada ya ujuzi wa mafataki kutumika kwenye jukwaa na bendi ya muziki wa rock ya Great White mwaka 1980 kushika moto kwenye povu la kudhibiti sauti ukutani na kwenye dari.
Na ajali ya uchomeleaji imeripotiwa kutokea mwaka 2000, moto katika klabu mjini Luoyang, nchini China na kuua watu 309.

No comments:
Post a Comment