Kamanda David Misime. |
Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada ya Uuguzi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu John mkoani Dodoma ameuawa akitoka kujisomea.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, David Misime alimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Lydia Mzima (57) na kuongeza kuwa mwili wa mwanafunzi huyo uligundulika jana asubuhi karibu na chuo hicho.
Akielezea tukio hilo alisema kwa kawaida mwanafunzi huyo huondoka na mwenzake ambaye wanakaa pamoja na kwenda kujisomea lakini usiku wa kuamkia jana hakuwapo na hivyo kuondoka pekee yake.
Alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mwanafunzi huyo alikatwa na kitu chenye makali kichwani.
Kamanda Misime alisema pamoja na kukatwa na kitu hicho pia paja la kulia lilionekana kunyofolewa na mnyama asiyejulikana.
Alisema kwa mujibu wa taarifa za awali mnyama aliyemnyofoa mguu ni fisi lakini bado wataalamu wanaendelea na uchunguzi ili kuthibitisha hilo.
Hata hivyo, Kamanda hakuonesha kama kulikuwa na dalili za mwanafunzi huyo kubakwa kabla ya kuuawa na Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ikiwa ni pamoja na kuimarisha doria katika eneo hilo la chuo.
Kamanda aliwaomba wananchi wenye taarifa yoyote juu ya tukio hilo kutoa taarifa hizo kwa Jeshi hilo ili wauaji wapatikane na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya ukisubiri uchunguzi wa madaktari.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Gabriel Mwaluko alithibitisha tukio hilo la mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu.
Alisema hayo yote yanatokana na chuo kukosa mabweni ya wanafunzi kulala jambo ambalo linafanya wanafunzi wengi kwenda kupanga mitaani na kukubwa na matukio mbalimbali.
Wakizungumza kwa masikitiko na mwandishi jana, baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho walisema marehemu alikuwa muuguzi katika hospitali ya Kilimatinde, Manyoni mkoani Singida.
Mei mwaka jana, wanafunzi wa chuo hicho waligoma kuingia madarasani hadi wawasilishe malalamiko yao kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kupigwa nondo, kuibiwa vitu kulawitiwa na hata kubakwa.
Walisema sababu nyingine inayochochea matukio hayo ni chuo kukosa uzio na hivyo kurahisisha mwingiliano wa watu na wanachuo.
Hivi karibuni wanachuo wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dar es Salaam waliandamana wakipinga kukithiri kwa vitendo vya wizi, ubakaji na ulawiti katika hosteli zao zilizoko Kigamboni.

No comments:
Post a Comment