Mwanamke ambaye kwa maoni ya walio wengi kwamba wanaume wanavutiwa na mahipsi yake ni Mikel Ruffinelli, mama wa watoto wanne mwenye uzito wa zaidi ya kilo 190 ambaye kipimo cha upana wake kinafikia futi za mzingo nane.
Mikel mwenye miaka 39 ambaye anaishi mjini Los Angeles, kwa uhalisia ni mpana kuliko urefu wake, lakini anasema hangependa njia nyingine yoyote mbadala kuhusu jinsi alivyo.
"Naipenda shepu yangu na sioni sababu ya kujinyima chakula sababu sitaki kupata matatizo ya kiafya," anafafanua Mikel, ambaye ana uwiano mdogo wa inchi 40 sehemu ya kiuno chake. "Wanaume hawavutiwi na visichana vyembamba, wanapenda wenye maumbile ya glasi kama la kwake."
Ingawa watu kama Jennifer Lopez, Kim Kardashian na Beyonce wote wanaweza kuafikiana, hawatakiwi kukabiliana na aina ya changamoto ambazo Mikel anakutana nazo kila siku.
Huku akilazimika kupita kwenye milango yote kwa upande-upande, Mikel huendesha lori sababu hatoshi kwenye gari ndogo. Nyumbani, mwanamke huyo mwenye mahipsi mapana zaidi duniani analazimika kukaa kwenye kiti kilichotengenezwa kwa chuma na kulala katika kitanda chenye upana wa futi saba.
Shabiki mkubwa wa Mikel ni mumewe, Reggie Brooks mwenye miaka 40, mtaalamu wa kompyuta. Wamekuwa wakiishi kwenye ndoa kwa miaka 10 sasa na Mikel anasema kwamba Reggie amegundua kwamba umbo lake hilo lisilo la kawaida linavutia mno na kumsifia kila siku jinsi alivyo mrembo.
Mikel hakuzaliwa na umbo hilo lililokubuhu, akiwa msichana alikuwa mwenye umbile la kimichezo na uzito wa kilo 64 ingawa alikuwa na mahipsi makubwa- mwenendo anaosema ulikuwapo kwenye familia yao.
Akiwa na miaka 22, Mikel alipata mtoto wake wa kwanza, Andrew, ambaye sasa ana miaka 19, kutoka kwenye mahusiano yake ya awali, na kwamba hapo ndipo alipoanza kuongezeka uzito. Kutoka kilo 83 na saizi 14, aliongezeka kwa kasi hadi kufikia kilo 108 na saizi 18.
Kisha akakutana na Reggie na kwa zaidi ya muongo uliofuata akapata watoto watatu zaidi: Destynee mwenye miaka 13, Autumn miaka 9 na Justyce miaka 7. Mahipsi yake yalijaa hadi kufikia kilo 190 na saizi 30.
"Nimesitisha kubeba ujauzito. Sioni kwanini tena uzito uongezeke kwenye mahipsi yangu, ingawa, nimekuwa nakula mno," alilieleza jarida la Closer.
Mikel, ambaye anasomea digrii ya udaktari, amekuwa na mlo maalumu wa kiafya ambao unampatia kalori 3,000 kwa siku.
"Inaonekana kama imezidi kuwa na kalori 3,000, lakini kwa mtu wa saizi yangu, si chochote.
"Ninapata kifungua kinywa cha mayai mawili sambamba na soseji na viazi vichache. Mchana nakaanga samaki na chipsi, lakini usiku ndio mlo wangu mkubwa," anakiri Mikel.
"Napenda kutengeneza kuku wa kuchoma na wali au viazi vya kupondwa. Nina napakua sehemu kubwa - lakini mimi sio mroho."
Wakati umri wake ukisonga kwa kasi, Mikel anasema amekuwa akifurahia sana shepu na saizi yake.
"Siku zilizopita, nilikuwa nikijihisi vibaya kuhusu mahipsi yangu na kujaribu kushindia maziwa tu, lakini haikusaidia kitu. Huku umri ukisonga mbele, nikajifunza kuupenda mwili wangu na sasa siogopi kuuonesha hadharani."
Kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita huku kujiamini kwake kukiongezeka amepigwa picha za mitindo kwa ajili ya mtandao wa Wanawake Wakubwa Warembo na kujipatia zaidi ya Dola za Marekani 1,000 kwa kila picha.
Mikel anafanya jitihada kujiweka mwenye afya na japo kukimbia ni tatizo, lakini anafurahia michezo ya kwenye maji.
"Sitaki kuwa bonge, lakini sitaki kupoteza mahipsi yangu. Naonekana wa kipekee. Naamini nashawishi wanawake kufikiri, "Anafurahia mwili wake na mimi naweza kuwa kama vile!"

No comments:
Post a Comment