MTANGAZAJI MKONGWE ASHITAKIWA KWA MASHAMBULIO ZAIDI YA UBAKAJI...

Stuart Hall alivyo sasa akiwa nje ya mahakama na akiwa na mke wake katika miaka ya 1970 (kulia).
Stuart Hall ameshitakiwa kwa mashambulio zaidi ya ubakaji katika historia ikiwamo kumbaka msichana na mashitaka 14 ya udhalilishaji watoto hadi wenye umri mdogo wa miaka tisa.
Mtangazaji huyo mkongwe, mwenye miaka 83, alikamatwa juzi pale alipofika kwenye kituo cha polisi cha Lancashire kwa miadi kuhusu madai ya kupitiliza kipindi cha miaka 19.
Ubakaji huo unadaiwa kufanyika mwaka 1976 kwa msichana wa miaka 22 na mashitaka ya shambulio hilo la udhalilishaji na kuripotiwa kuwa yalifanywa kati ya mwaka 1967 na 1986. Inawahusu wasichana kumi wenye umri wa miaka kati ya tisa na 16.
Mtangazaji huyo wa Redio na televisheni ya BBC alipandishwa mahamamani mapema mwezi huu kujibu tuhuma za mashambulio mengine matatu ya ubakaji.
Taarifa ya polisi wa Lancashire ilisema: "Kufuatia majadiliano na ofisi ya mashitaka, mzee huyo wa miaka 83 jioni hii amefunguliwa mashitaka ya moja la ubakaji na 14 ya udhalilishaji."
Hall tayari alishashitakiwa Desemba kwa kudhalilisha wasichana watatu.
Mashitaka haya ni yamejumuisha madai ya shambulio la msichana wa miaka minane, miaka 11 na mwanamke ambaye wakati huo alikuwa na miaka 16. Madai hayo ni ya kati ya mwaka 1974 na 1984.
Stuart, ambaye anafahamika kwa utangazaji wake mahiri wa soka kwenye kituo cha Radio 5 Live, aliachiwa kutoka mahabusu na apewa dhamana ambapo anatakiwa kufikishwa kortini mwezi huu kukabiliana na mashitaka matatu.
Lakini sasa kesi hiyo itakwenda mbele ya hakimu mjini Preston hapo Aprili 16. Tayari ameonekana hana hatia.
Na, katika mwanga wa madai mapya yaliyoibuliwa dhidi yake, amepatiwa dhamana kabla ya kufikishwa mbele ya hakimu, tena mjini Preston, Februari 7.
Desemba, mwajiri wa Stuart katika Radio 5 Live ya BBC alitangaza mkongwe huyo hatofanya kazi hapo wakati uchunguzi wa polisi ukiendelea.

No comments: