HUU NDIO MOTO UNAOWAKABILI WACHAFUZI WA MAZINGIRA KINONDONI...

Meya usuph Mwenda.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imesema itaanza kutoza faini wakazi watakaochafua mazingira kwa kutupa taka ovyo ikiwa ni kampeni maalumu ya kuweka safi mazingira.
Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda alisema hayo katika hafla ya kukabidhiwa msaada wa vifaa 100 vya kubebea taka vyenye thamani ya Sh milioni 3.5. Benki ya ABC ndiyo iliyotoa vifaa hivyo.
Alisema watatoza faini kuanzia Sh 10,000 hadi Sh 50,000 kulingana na kosa na kwamba  vikundi vya vijana watakaosimamia kampeni hiyo vimeundwa.
“Huu ni mwendelezo wa kampeni tuliyoizindua ya kuweka safi Manispaa yetu. Hivyo wakazi wa Kinondoni wanapaswa kuvitunza vifaa hivi sambamba na kutunza usafi wa mazingira, vinginevyo manispaa haitasita kuwatoza faini.” alisema.
Alisema wana mpango wa kuwa na vifaa 500 vya kubebea  taka ambavyo vitasambazwa katika kata zote 34. 
Ofisa Masoko wa benki hiyo, Evelyn Auguste alisema msaada huo ni sehemu ya marejesho ya faida ya benki hiyo kwa jamii.

No comments: