MWANAMKE ALIYEBAMBWA NA KILO 5 ZA COCAINE AHUKUMIWA KIFO...

Lindsay Sandiford (kulia) akiwa mwenye mawazo katika selo nchini Bali.
Mwanamke wa Uingereza aliyehukumiwa kifo kwa kusafirisha dawa za kulevya huko nchini Bali ameangukia kwenye mfadhaiko mkubwa, ambao umemwacha akiwa hawezi kula au kulala huku akiwa amedhoofika ndani ya selo yake iliyojaa wafungwa, mwanasheria wake alisema jana.
Lindsay Sandiford, mwenye miaka 56 'amekwisha na kupotea kabisa' tangu jopo la majaji kumhukumu adhabu ya kifo kwa kupigwa risasi kwa kujaribu kusafirisha karibu kilo tano za cocaine zenye thamani ya Pauni za Uingereza milioni 1.7 kupitia Uwanja wa Ndege wa Denpasar mwaka jana.
"Ametikiswa mno kisaikolojia na hukumu hiyo," alisema mwanasheria Esra Karokaro, ambaye alikiri kwamba naye pia amebakia kwenye hali ya mshituko kuhusu hukumu hiyo ya kifo, sababu upande wa mashitaka ulipendekeza kifungo cha miaka 15 tu jela.
Imefahamika wafungwa kadhaa wanawake katika selo iliyojaa ya Lindsay ambao wanaweza kuongea kiasi Kiingereza wamekuwa wakijaribu kumfariji lakini amekata tamaa mno kiasi kwamba amewanyamazia tu.
Amekataa kula chakula cha jela na amekuwa akitumia muda mwingi tangu hukumu hiyo akilala kwenye kipande cha nguo katika sakafu ya selo iliyopo Jengo W - kitengo cha wanawake - cha gereza lenye sifa mbaya la Kerobokan.
Esra alisema kwamba ingawa Lindsay alifahamu kwamba kiwango cha cocaine alichojaribu kusafirisha kuingia nchini humo adhabu yake ni kifo, ametumia wiki za hivi karibuni kukaa na ndugu zake akielezea kwamba anatakiwa kutumikia muda wa kifungo gerezani na si kukabiliana na kufa kwa kupigwa risasi.
Juzi mtaalamu wa matukio ya uhalifu Bali alisema Lindsay alikuwa 'ni sura iliyozoeleka' katika dunia ya dawa za kulevya na kufanya safari za mara kwa mara kutoka India akisafirisha bangi.
Kathryn Bonella, mwandishi wa kitabu cha Snowing katika Bali, kuhusu uhalifu wa kisiwa hicho duniani, alisema Lindsay aliingia nchini humo akitokea Uingereza kupitia India.
Akiongeza na gazeti la Times alisema: "Alikuwa akiingiza bangi hapa kutoka India na kuuza kwa mmoja wa watu wangu, lakini hivi karibuni akahamia kwenye cocaine.
"Nawafahamu wafanyabiashara wengi wakubwa magharibi wa dawa ambao wameingia kwenye kisiwa hiki pale walipogundua amelipuka na kugeuka kuwa panya."
Rufani ya Lindsay inatarajiwa kuwasilishwa ndani ya siku saba inaweza kumburuta mahakamani kwa miaka kadhaa na kwa kipindi chote hicho akifahamu hukumu ya kifo itaendelea kumwandama na hatimaye kutekelezwa.
Endapo rufani zote zitashindwa anaweza kuomba huruma ya Rais lakini hasi hapo hakuna uhakika atapatiwa muda huo pale atakapotolewa kutoka kwenye selo yake kabla ya mapambazuko na kupelekwa kwenye uwanja wa taka - kwa kawaida kiunga cha miti ya matunda - akifunikwa macho kwa kitambaa na kupigwa risasi kwenye moyo wake.
Hata kama Lindsay anapatiwa aina ya kazi za kawaida katika gereza, mwanzo wa siku yoyote itamletea ufahamu wa kwamba mwisho wa yote ataishia kwenye kifo.
Wanawake wengi walioko kwenye selo moja naye, wanalala kama anavyofanya yeye kwenye sakafu, miili yao ikigusana sababu ya mazingira ya msongamano, wamo humo kwa mashitaka ya dawa za kulevya, ukahaba na wizi.
Mende na wakati mwingine panya wanakimbizana juu ya miili yao wakati wa usiku na kuna kiasi kikubwa sana cha mbu. Mazingira mabovu ya usafi yamechangia matatizo ya afya, licha ya kwamba wafungwa wanaruhusiwa kutoka nje ya selo zao kufanya mazoezi na kazi za kawaida.
Anachoweza kutarajia Lindsay katika siku za usoni ni kutembelewa na dada yake, Hillary Parsons, ambaye alikuwapo mahakamani wakati wa hukumu, mshituko kuhusu adhabu hiyo ya kifo ukiwa umetanda kwenye uso wake.
"Dada yake ameniuliza kuhusu taratibu za kisheria zinazotakiwa kukata rufani," alisema Karokaro. "Kama unavyoweza kufikiria, dada yake Lindsay pia ameona hili lilivyo gumu kushughulikia."
Alisema kwamba kwa wakati huu, sambamba na kuanza kupinga, yeye na Parsons wamekubaliana kushughulikia kumtoa Lindsay kwenye mfadhaiko wake hivyo kuweza kukubali hali kwamba hakuna kinachoweza kubadilika kwa kipindi kirefu sana.

No comments: