SITTA ASEMA HANYAMAZI NG'O, SUMAYE KUTOA LAKE LA MOYONI...

Samwel Sitta
Uchaguzi unaoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeelezwa kuwa utabiri mwema kwa chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kutokana na kuingiza sura mpya huku vigogo wakibwagwa.
Aidha, baadhi ya waliong’ara katika uchaguzi huo wametabiriwa neema kushika nafasi za juu katika Serikali ukiwamo urais mwaka 2015 ikiwa watakuwa tayari kusafisha madoa waliyonayo.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Dk Benson Bana alisema jana kuwa CCM imedhihirisha ni chama dume, chenye demokrasia na ukomavu kisiasa.
Akifafanua, alisema: " Uchaguzi unadhihirisha wazi kuwa CCM bado inadunda na dhana ya kujivua gamba inatekelezwa, watu zaidi ya 5,000 walipitishwa Dodoma huku sura mpya zikijitokeza, miongoni mwao ni vijana, wazee hata wakulima".
Dk Bana alisema hatua hiyo imedhihirisha mianya ya rushwa kudhibitiwa ndani ya chama hicho, baada ya kuona magwiji wa siasa akiwamo Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, wakiangushwa, jambo linaloashiria hakubaliki kuwania urais.
"Hakuna asiyejua mbio za Sumaye kutaka urais, sasa kama jimbo la Hanang watu wachache wamekukataa, si rahisi Watanzania wakupe urais, namshauri sasa arejee kutumika katika nafasi yake ya siasa kama Waziri Mkuu mstaafu, maana Watanzania wameamua kufanya mabadiliko," alisisitiza Dk Bana.
Kuhusu madai hayo, alipoulizwa Sumaye jana, alisema, "najua unataka habari ya uchaguzi, sasa hivi sisemi lolote ila nitakuja Dar es Salaam kati ya siku mbili au tatu hivi, utaniuliza na hilo swali lako nitakapozungumza nanyi waandishi wa habari."
Akizungumzia harakati za urais mwaka 2015 kutokana na uchaguzi huo wa CCM, Dk Bana alisema CCM itang’ara katika uchaguzi ujao ikisimamia mweleko wa sasa, lakini hatima yake imesimama katika mambo mawili; Katiba mpya na uteuzi wa atakayepeperusha bendera kuwania urais.
"Uchaguzi 2015 tutarajie mambo makuu mawili; Katiba mpya ndio pekee itatoa mwelekeo wa kitakachotokea, lakini pia CCM inateua nani kuwania urais wakati huo, hii itabadili mtizamo wa siasa, wakiteua vizuri, watawafunika wapinzani," alisisitiza Dk Bana.
Dk Bana alivunja ukimya na kueleza wazi kuwa, hivi sasa ndani ya CCM kuna mtu anayenukia urais, ila bado ana madoa anayopaswa kuyasafisha ili akubalike. Alimtaja mtu huyo kuwa ni Waziri Mkuu wa zamani ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.
Hata hivyo, Dk Bana aliitaka CCM iwaadabishe baadhi ya wanachama, baadhi ni viongozi wa nchi akiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta na Peter Kisumo (Mdhamini wa CCM) kwa alichodai, wanazungumza bila kufuata utaratibu.
"Hawa wana kambi zao ndani ya chama, wanataka kumvuruga Katibu Mkuu Mukama (Wilson) kwa kauli zao, wasipewe nafasi waadabishwe kurejesha nidhamu," alihimiza Dk Bana aliyekuwa akitoa maoni yake kuhusu uchaguzi unaoendelea CCM.
Akijibu tuhuma hizo jana, Sitta alisema: "Nimezoea, kauli zangu hazijawahi kuwafurahisha hata siku moja mafisadi, nataka wajue hivi; nitazungumza mpaka tone la mwisho la pumzi yangu, nimefundishwa kukemea maovu na Baba wa Taifa (Mwalimu Julius Nyerere)".
Sitta alijigamba kuwa, alijiunga na TANU Oktoba 3, 1960 akiwa kidato cha tatu na sasa ni miaka 52 ndani ya chama, hajavunja utaratibu wowote katika kukemea maovu na wanaotaka anyamaze, anawakera kwa kuwa amewagusa.
"Sitachoka kusema mafisadi, maana wanaharibu nchi yetu, hata Ilani ya chama inanilinda nikemee maovu, sisubiri ruhusa ya mtu yeyote, nani asiyejua kuwa Chenge (Andrew-Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM) ni mtuhumiwa, haiingii akilini eti amepita bila kupingwa Bariadi, watu 11 waliochukua fomu wamefutikia wapi?" Alihoji Sitta.
Sitta, Spika mstaafu alipotakiwa kufafanua hoja hiyo, alisisitiza kuwa inajulikana wazi ndani ya chama na wachache wenye ujasiri kama yeye, ndio wana uwezo wa kusema na kusisitiza kwamba hatanyamaza mpaka pumzi yake ya mwisho.
Hata hivyo, alikiri kuwa uchaguzi wa CCM umekwenda vizuri ila hivi sasa yapo baadhi ya maeneo bado rushwa inatumika kupindisha matokeo na kusisitiza kwamba ikiwa rushwa itakemewa ndani ya chama na viongozi halali wakapatikana, hata dawa hospitalini zitapatikana na ndilo tamanio la wapenda maendeleo.
Dk Bana aliendela kumshauri Rais Jakaya Kikwete kutumia muda mwingi kuzungumza na wanachama katika ngazi za wilaya, kwa kuwa anakubalika kwa zaidi ya asilimia 60 hadi 70 na nguvu ya chama ni mwenyekiti.
"Hakuna chama bila mwenyekiti, kitayumba, Kikwete anakubalika, binafsi afanye ziara kuzungumza na wanachama, asisubiri kuonekana wakati wa uchaguzi bali afanye ziara kuimarisha chama," alishauri Dk Bana.
Alisema mpaka sasa zaidi ya asilimia 51 ya wagombea wa uchaguzi unaoendelea ni wasomi kuanzia Stashahada na Shahada mbalimbali, kinachogomba upinzani ni watu wachache wanaopiga kelele na kusahau kujenga vyama vyao.
"Tatizo la Upinzani ni kwamba, wamegeuka kuwa wanaharakati wa kuitisha maandamano ya mpaka kieleweke, nini kieleweke? Tena wachache ndio wanapiga kelele, wanapaswa kurudi kuwa wanasiasa na si wanaharakati, wawaache Tamwa (Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake) na wengine," alikazia Dk Bana.
Alisema ni kwa misingi hiyo, anarejea kauli yake kuwa bado ni ndoto kwa upinzani kushika Dola kwa kuwa wamekuwa na kazi ya kuishambulia Serikali kwa kutumia watu wachache machachari na kusahau kuimarisha ndani na kufanya uchaguzi wao usiwe na mvuto wala vuguvugu kutokana na ufinyu wa demokrasia.
"Watu hawataacha kusema kuhusu uchaguzi katika upinzani kuwa watu wanapeana vyeo, kwa sababu ya ushemeji, hili litafutika ikiwa demokrasia ya kweli itaachwa ifanye kazi ndani, wasipige kelele nje wakati ndani hakujakaa sawa," alishauri Dk Bana.
Alishauri wapinzani kuiga demokrasia iliyotumika ndani ya CCM na kuhakikisha kuwa mikakati yao kupitia M4C (Chadema) na V4C (Cuf), zinazaa matunda ya kuimarisha vyama vyao.
Katika hatua nyingine, Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Method Kilaini ametoa maoni yake kuhusu uchaguzi huo wa CCM na kukipongeza chama hicho akidai kimeonesha ukomavu wa kisiasa.
"Wale walioshindwa hawapaswi kupiga kelele na kama wakipiga sana, watu watahoji walikuwa si washindani bali kuna kitu walikuwa wanatafuta. Mshindani siku zote anakubali kushindwa," alishauri Kilaini.
Wilayani Bariadi Juliana Mahongo alitetea nafasi yake ya Mwenyekiti huku Andrew Chenge akipita bila kupingwa katika nafasi ya ujumbe wa NEC na Masunga Yabuyeze akitetea nafasi yake ya Katibu Mwenezi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Erasto Sima aishinda ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na wajumbe wengine Tina Chenge, Gasper Mjuna, Rachael Subanda na Masanja Kidogosa.
Pia wilaya ya Itilima ilipata Mwenyekiti wa CCM ambapo Mabula Mohamed alichaguliwa huku ujumbe wa NEC ukienda kwa Daud Njalu ’Nsagali’, na John Nkululu alichaguliwa kuwa Katibu wa Uchumi na ukatibu mwenezi ukienda kwa Mang’ombe Gwalugwa.
Katika wilaya ya Busega aliyechaguliwa kushika nafasi ya Mwenyekiti ni Mshoni George, huku uNEC ukienda kwa Raphael Chegeni na Katibu Mwenezi akichaguliwa Raphael Babasha.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya, alichaguliwa ujumbe wa Mkutano Mkuu Taifa na wajumbe wengine wakiwa ni Hamis Haule, Josia Mgemu, John Mkale na Mikinesi Mahela.
Wilayani Maswa Mwenyekiti wa Wilaya Peter Bunyongoli alichaguliwa tena kuendelea na wadhifa wake na Aron Mboje akachaguliwa kuwa mjumbe wa NEC.
Wajumbe watano wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ni Masanja Mpiga, Pili Kidosela, Amina
Almasi, Thobias Kadome na Mercia Emmanuel.

215 comments:

«Oldest   ‹Older   201 – 215 of 215
Anonymous said...

I dugg some of you post as I cogitated they were extremely helpful very beneficial.

Anonymous said...

Hello! This is my first visit to your blog! We are a collection of volunteers and starting a new
initiative in a community in the same niche. Your blog provided us valuable
information to work on. You have done a outstanding job!

Anonymous said...

There is perceptibly a bunch to identify about this. I
assume you made various good points in features also.

Anonymous said...

Really nice style and design and fantastic content material, hardly anything else we want :
D.

Anonymous said...

Hi there! I could have sworn I've been to this website before but after browsing through some of the post I realized it's new
to me. Nonetheless, I'm definitely glad I found it and I'll be book-marking and checking back often!

Anonymous said...

Excellent read, I just passed this onto a friend who was doing a little research on that.
And he just bought me lunch because I found it for him smile Therefore let me rephrase that:
Thank you for lunch!

Anonymous said...

I as well as my buddies were actually analyzing the great tactics located on your site and suddenly got a horrible feeling I
never thanked the web site owner for those strategies.
Those ladies came absolutely passionate to read through all of
them and already have clearly been using these things.
Appreciate your being quite kind as well as for having varieties of impressive information millions of individuals
are really eager to understand about. Our own honest regret for
not saying thanks to sooner.

Anonymous said...

Hi there Dear, are you genuinely visiting this web
page on a regular basis, if so after that you will without doubt take nice knowledge.

Anonymous said...

I'm not sure the place you're getting your information, however great topic.
I needs to spend some time finding out much more or working
out more. Thank you for excellent information I
was in search of this information for my mission.

Anonymous said...

Hello.This post was extremely motivating, particularly because I was investigating for thoughts on this topic last
week.

Anonymous said...

This is a really good tip particularly to those fresh to the
blogosphere. Short but very accurate info? Appreciate your
sharing this one. A must read article!

Anonymous said...

You really make it appear so easy with your presentation however I to find this topic to be really something that I think
I might never understand. It seems too complex and very vast for me.
I'm taking a look forward on your subsequent publish, I will
try to get the hold of it!

Anonymous said...

Howdy, i read your blog occasionally and i own a similar one and i was just wondering if you get a lot
of spam responses? If so how do you prevent it,
any plugin or anything you can suggest? I get so much lately it's driving me
mad so any assistance is very much appreciated.

Anonymous said...

Some genuinely interesting information, well written and loosely user pleasant.

Anonymous said...

How much do you think this tattoo will definitely cost?
This will end up being my second tattoo. I understand every artist varies
I just really want a ballpark idea. https://ibb.co/kKLdrd Just how much will it cost to
get rid of in 5 years may be the real question.

«Oldest ‹Older   201 – 215 of 215   Newer› Newest»