Mwanamke mwalimu msaidizi ambaye alipachikwa jina la 'mwindaji ngono' anakabiliwa na adhabu ya kifungo jela baada ya kukiri kujihusisha na wanafunzi wavulana baada ya shehere za kumaliza mwaka.
Emma Webb mwenye miaka 41, mama wa watoto wawili aliye katika ndoa, alikuwa akituhumiwa kwa kudhalilisha nafasi yake ya uaminifu na wavulana watatu katika shule ya sekondari ambako anafanya kazi, ambayo haiwezi kuwekwa bayana kwa sababu za kisheria.
Akipandishwa kizimbani ambako alikiri mashitaka 16 ya kusababisha wavulana wa umri kati ya miaka 15 na 17 kujihusisha na matukio ya ngono.
Mara yake ya kwanza kufikishwa kortini Juni mbele ya hakimu wa mahakama ya Reading, Mwendesha Mashitaka Helen Gambrill alimuelezea Emma kama 'mwindaji ngono'.
Emma alikuwa akituhumiwa kulala na mmoja wa wanafunzi zaidi ya mara 12 kwa nyakati tofauti na kufanya naye vitendo vya ngono pamoja na kijana mwingine, ikiwa ni pamoja na kubusiana na kupapasana.
Alimtumia pia mmoja wa wavulana hao picha alizojipiga wakati akifanya vitendo vya ngono mwenyewe, mahakama ilielezwa.
Emma, ambaye alikuwa akifanyakazi kama mshauri na msimamizi wa darasa, alisimamishwa kazi Mei 31 baada ya wenzake kuripoti mashaka yao kuhusu ukaribu wake na baadhi ya wanafunzi. alikamatwa baada ya mmoja wa wanafunzi hao kumripoti kwa wazazi wake na shuleni.
Mumewe Andy, fundi bomba ambaye anaishi naye huko Woodley, Berkishire, alikuwa akifuatilia kesi hiyo akiwa upande wanaoketi watu wengine mahakamani hapo. Imefahamika kwamba wanandoa hao wamekuwa pamoja kwa miaka 18 iliyopita.
Juzi, Jaji wa Mahakama Kuu ya Reading, John Reddihough alimweleza ingawa anaweza kupewa 'sifa zote' kwa kukiri kosa mapema kabisa, hawezi kuepushwa na kifungo.
Alirejeshwa rumande na atahukumiwa mwezi ujao.
Mmoja wa majirani zake alisema: "Nimemfahamu Emma tangu akiwa mdogo. Ni mtu wa mwisho kabisa duniani kumhisi kuwa anajihusisha na vitu kama hivi."

No comments:
Post a Comment