"MTOTO WA RAMBO ALIKUFA KWA MSHITUKO WA MOYO"...

Mtoto wa kiume wa Sylvester Stallone, Sage Stallone, alifariki kutokana na mshituko wa moyo ...na kwamba hakuna dawa za kulevya zilizopatikana katika mfumo wake wa damu, imefahamika.
Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Los Angeles imebainisha Sage alikuwa kwa sababu za kawaida. Kuhusu sababu za kupatwa mshituko wa moyo, imeelezwa kwamba kulikuwa na uthibitisho alikuwa na maradhi ya moyo.
Chanzo cha habari chenye uhusiano na Mkemia Mkuu kimeeleza ...ilikuwa 'si kawaida' kwa mtu wa rika la Sage, miaka 36, kuwa na matatizo ya moyo kwa kiwango hicho, lakini hicho ndicho kilichomuua.
Mwili wa Sage ulipatikana Julai 13, lakini inawezekana kuwa alifariki siku kadhaa kabla.

No comments: