Trafiki alikuwa akipita gari moja hadi jingine kwenye foleni ndefu maeneo ya Kinondoni Mkwajuni ndipo alipofika kwenye gari langu. Nikamuuliza, "Afande, nini kinachoendelea?" Trafiki akanijibu, "Kuna mpuuzi mmoja anatishia kutaka kujichoma moto, hivyo tunapita gari kwa gari kukusanya michango!" Nikaendelea kuhoji, "Michango? Kwani mpaka sasa mmeshapata kiasi gani?" Trafiki akanijibu, "Karibu madumu kumi ya petroli!" Balaa…
No comments:
Post a Comment