'DEMU' WA PREZZO AFUNGASHA VIRAGO BIG BROTHER AFRICA...

Mshiriki kutoka Nigeria katika Shindano la Big Brother Africa mwaka huu, Goldie amepigiwa kura ya kutoka kwenye jumba hilo jana.
Dada huyo ambaye alikuwa karibu sana na mshiriki kutoka Kenya, msanii wa kizazi kipya Prezzo, kiasi cha kufikia hatua ya kuvishana pete inayoaminika kuwa ya uchumba, alibubujikwa na machozi pale alipopewa nafasi ya kuona mchakato mzima wa upigaji kura kutoka kwa washiriki wenzake kiasi cha kushindwa kuamini rafiki zake ambao walimtaja walipohojiwa na Big Brother na kupewa nafasi ya kuchagua mshiriki wanayetaka atolewe.
Baada ya Goldie ambaye amedumu kwenye jumba hilo kwa wiki 10 kutolewa, Prezzo alionekana mwenye mawazo huku akifarijiwa na washiriki wenzake kadhaa.
Shindano hilo limefikia patamu ambapo tofauti na mwanzo ambapo washiriki waligawanywa katika makundi mawili ya Upville na Downville, sasa wote wamewekwa sehemu moja na pia kila mshiriki anapigiwa kura kivyake tofauti na mwanzo ambapo walikuwa kama patna.
Shindano hilo hurushwa na DStv kupitia chaneli yake ya Africa Magic namba 198.

No comments: