CHEKA TARATIBU...

Bibi mmoja baada ya kukaa kwa siku kadhaa bila kusikia sauti ya bibi mwenzake nyumba ya jirani, ndipo akaamua kumtuma mjukuu wake kwenda kumjulia hali. Bibi akamwambia mjukuu wake, "Nenda kwa bibi wa jirani kamuulize ana miaka mingapi?" Mjukuu akaenda na baada ya dakika kadhaa akarejea. Bibi akamuuliza tena, "Vipi umemkuta mzima? Mjukuu akajibu, "Ndiyo bibi, ila ana hasira sana na wewe." Bibi akahoji, "Nimemkosea nini?" Mjukuu akajibu, "Kasema miaka yake wala haikuhusu." Balaa...

No comments: