ALIYECHEKELEA 'KIFO' CHA MUAMBA KWENDA JELA...

Liam Stacey, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Swansea anakabiliwa na hukumu ya kifungo jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutuma ujumbe wa kashfa dhidi ya mchezaji wa Bolton Wanderers, Fabrice Muamba ambaye alianguka ghafla uwanjani baada ya kushindwa kupumua katika mechi ya robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Tottenham Hotspurs kwenye Uwanja wa White Hart Lane, mjini London Jumamosi iliyopita.
Imeelezwa mahakamani kwamba, Stacey alituma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter uliosomeka, "[Cheka kwa sauti] ****Muamba. Amekufa!!!" akionesha kufurahia tatizo lililomkuta Muamba, muda mfupi baada ya kuanguka uwanjani. 
Mchezaji huyo bado yuko hospitalini chini ya uangalizi maalumu na taarifa za karibuni kutoka klabuni kwake zinasema sasa anaweza kupumua mwenyewe bila msaada wa mashine maalumu.
Juzi Stacey mwenye miaka 23, mwanafunzi wa baiolojia chuoni hapo alikaribia kumwaga machozi kortini wakati ujumbe aliotuma kwenye Twitter ulipokuwa ukisomwa tena. Mwendesha mashitaka, Lisa Jones aliiambia mahakama, "Fabrice Muamba na iliaminika kuwa amekufa. Muda mfupi baadaye, Stacey alituma ujumbe kwenye Twitter: "[Cheka kwa sauti], **** Muamba. Amekufa."
"Wafuatiliaji wengi wa Twitter walimtumia ujumbe mbalimbali wa kumlaani lakini yeye Stacey hakukaa kimya na kuamua kuwajibu akitetea alichokiandika kwenye mtandao huo."
Mwendesha mashitaka aliendelea, "Ujumbe aliotuma uliwalenga watumiaji wa Twitter wengi wao wakiwa watu weusi, na ulikuwa wa hatari ambao haukutakiwa kuwekwa mtandaoni."
Mwanasoka wa zamani wa England, Stan Collymore, mmoja wa watu waliotoa taarifa polisi kuhusu ujumbe huo wa Stacey, aliwaeleza watumiaji wengine wa mtandao huo kuwa maofisa wa polisi wanachunguza pia taarifa mbalimbali zilizotumwa kwenye mtandao huo.
Mtumiaji mmoja aliyejisajili kama Chet Walken kutoka Houston, Texas, aliandika ujumbe mbalimbali za kibaguzi akiwashutumu baadhi ya wanasoka waliotaka afungiwe kushiriki kwenye mtandao huo.
Mlinzi wa timu ya Queen's Park Rangers, Anton Ferinand na beki wa Sunderland, Titus Bramble waliwaambia wafuatiliaji wao kuishawishi Twitter imfungie Walken kushiriki katika mtandao huo.
Kisha Walken akajibu, "Kwanini natumiwa baruapepe hizi? Inanifanya nitamani Marekani inemleta Hiltler aje kuwashikisha adabubyie wote msiokuwa na shukrani."
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Ryan Babel ameishutumu Twitter kwa kushabikia ubaguzi endapo haitamfungia Walken katika siku saba zijazo.

1 comment:

Anonymous said...

Hiki kijamaa kingenyongwa tu hakifai kuishi