JOHN CENA APATA AJALI YA GARI

Bingwa wa zamani wa mieleka wa WWE, John Cena amepata ajali baada ya gari lake kugongwa na lori la mizigo alfajiri ya leo, lakini imeelezwa kwamba amepata majeraha madogo na hivyo kutoathiri maandalizi ya pambano lake lijalo dhidi ya The Rock.
Cena alikuwa akiendesha gari aina ya SUV mjini Philadelphia ndipo alipogongwa na lori hilo. Habari zimesema kuwa atafanyiwa vipimo zaidi kuona kama amedhurika kwa ndani lakini kwa sasa haoneshi kama amepata madhara yoyote japo maumivu zaidi kwa kawaida huwa hayaishi kwa siku moja ama mbili.
Cena anajiandaa kumkabili The Rock Aprili Mosi, na pambano hilo linaonekana kuwa moja ya mapambano litakalovuta hisia kwa mashabiki katika historia ya mieleka.
Gari la John Cena likiwa eneo la tukio baada ya ajali kutokea mapema asubuhi hii.

2 comments:

Anonymous said...

Duh, ulikuwa mzinga babu kubwa. Kumbe hata ulaya madereva walu walu wapo!

chicky said...

Mbona kuna habari za kuwa anefariki hii ni kweli au habari za uzushi?