Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka amesema hisa ya
asilimia 10 kwa fidia watakayolipwa wananchi wa Kigamboni kupisha ujenzi wa mji
wa kisasa ni hiari.
Akizungumza
jana kwenye mkutano na madiwani wa kata sita zinazofikiwa na mradi huo,
watendaji wa kata na serikali za mitaa, Tibaijuka alisema pamoja na timu yake kuendelea kutoa elimu ya umuhimu wa hisa
za wananchi katika mradi huo, uamuzi wa kuwa na hisa au la utabaki kwa
mwananchi na haitakuwa lazima.
Tibaijuka
aliwataka viongozi na watendaji hao, kusaidia kutoa elimu ya wananchi kukatwa
asilimia 10 ya malipo ya fidia kama hisa mwananchi ili kuwapa uhalali wa
kuendelea kumiliki ardhi yao kisheria.
"Kama
ninyi madiwani mmekubali kukatwa sehemu ya fidia kama hisa ili muwe sehemu ya
umiliki wa ardhi, sasa kwanini msisaidie kuelimisha wananchi kukubali mpango
huo wenye manufaa siku zijazo?
“Si
sahihi viongozi kusema kila mtu achukue chake na ajijue mwenyewe wakati hatua
ya serikali ya kuwataka wananchi kuwa na hisa kwenye mradi huo ina faida kwa
wananchi,” alisema Profesa Tibaijuka.
Aidha
Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile alimtaka Profesa Tibaijuka kuhakikisha
wanawaeleza wananchi kwa kina fedha za hisa, zitaratibiwa na nani na wananchi
watapata manufaa gani.
Tubaijuka
alisema mchakato wa namna fedha hizo zitaratibiwa na taasisi itakayoratibu
unafanyiwa kazi na watalaamu na kuwa watu wote watakaokubali fedha zao kukatwa
kwenye hisa watapewa mikataba maalumu.
Aidha,
Profesa Tibaijuka alisema kuanzia Agosti 24, mwaka huu, watafanya mikutano ya
hadhara kwa ajili ya kuzungumzia mradi huo ambao awamu ya kwanza utafanyika
katika kata sita.
No comments:
Post a Comment