Mgogoro wa
ardhi umeibuka katika Kitongoji cha Majichumvi katika Kijiji cha Wami
Luhindo wilayani Mvomero, baada ya Maofisa Ardhi kuanza
upimaji viwanja.
Upimaji
huo unafanyika katika utekelezaji wa azimio la ukaguzi wa mashamba pori
yaliyotelekezwa kwa zaidi ya miaka 30 na wamiliki halali wa mashamba hayo.
Mwenyekiti
wa kitongoji hicho, Michael Mayalla, alisema hayo hivi karibuni katika
mkutano wa pamoja na wananchi wa kitongoji hicho, kuhusu hatma ya
mashamba hayo.
Mayalla
alisema ameshangaa kuona watu wa ardhi wakipima mashamba yao huku
wakijua kuna wakulima na wafugaji walihamishiwa humo kwa zaidi ya
miaka 10 iliyopita.
Alisema
alipowauliza maofisa hao kuhusu suala hilo, alipewa kauli kwamba mashamba hayo
yanamilikiwa na vigogo.
Ofisa
Ardhi wa Wilaya ya Mvomero, Majaliwa Jafari, alipoulizwa alisema kati ya 1980
hadi 1990, Serikali ilitenga ekari 60,000 za mashamba kwa ajili ya kilimo
cha nguvu kazi katika kijiji hicho.
Hata
hivyo alisema baadhi ya mashamba yalinunuliwa na baadhi ya
watu ambapo mengi hayakuendelezwa.
Kutokana
na hali hiyo, alisema Serikali ilitoa agizo la kutambua mashamba pori ili
yafutwe na kuangalia nini cha kufanya.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Wami Luhindo, Apolinali Kahumba, alisema katika kijiji hicho kuna
vitongoji sita kikiwemo cha Majichumvi,
ambapo pia alilalamika kuwa kilichofanyika ni halmashauri kutoshirikisha
uongozi wa kijiji, ndio kilichoibua mgogoro.
Alisema sheria
inaruhusu vijiji kugawa eneo lake kupitia Mkutano Mkuu wa Kijiji na kama
Serikali inahitaji eneo, ni lazima kijiji kishirikishwe.
No comments:
Post a Comment