Wanafunzi
wawili wa Shule ya Sekondari Kamuli wilayani Kyerwa mkoani Kagera wamekufa na
mmoja kujeruhiwa kwa kupigwa radi.
Makamu
Mkuu wa shule hiyo, Marco Renatus alisema juzi saa 7 mchana radi ilipiga nyumba
waliyokuwemo wanafunzi hao wakati mvua kubwa iliyoambatana na mawe na upepo
mkali iliponyesha.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alithibitisha kuwepo tukio hilo.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi jana, Mwalimu Renatus alitaja wanafunzi waliopoteza
maisha ni Amoni Aniseth (20) wa Kidato
cha Nne na Onesmo Odiro (14) wa Kidato
cha Kwanza.
Kwa
mujibu wa mwalimu huyo, radi ilibomoa ukuta wa chumba cha kwanza na chumba cha
pili, ambako wanafunzi hao walikuwa wamelala.
Amoni
alipoteza maisha baada ya kufikishwa
katika kituo cha afya Kamuli wakati Odiro alifariki saa 5 usiku katika Hospital
ya Isingiro wilayani Kyerwa.
Majeruhi,
Filibath Jackisonali wa Kidato cha Tatu aliruhusiwa jana baada ya
kupatiwa matibabu na kuonekana afya yake inaendelea vizuri.
Mganga
aliyekuwa zamu katika hospitali ya Isingiro, Letisia Masito alisema alimpokea
Onesmo juzi saa 2 usiku na kwamba akiwa katika harakati za kumpatia matibabu
saa 5 usiku, ndipo alipoteza maisha.
Hili
ni tukio la pili la radi ndani ya wiki moja baada Agosti 14 mwaka huu, watu
wawili katika kata ya Kanoni wilayani Karagwe, kupoteza maisha kutokana na kupigwa radi.
No comments:
Post a Comment