Serikali
i imesema itajipanga kuona namna ya
kukabili changamoto zinazokwamisha miradi mikubwa, inayoendeshwa
na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
kwa lengo la kubadilisha sura ya Jiji la Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda alisema hayo baada ya kutembelea miradi mitatu mikubwa
inayoendeshwa na NSSF, ikiwemo ujenzi wa
daraja la Kigamboni.
Miradi
mingine ni mradi wa nyumba za gharama nafuu inayojengwa Mtoni Kijichi na mradi
wa nyumba zaidi ya 7,000 uitwao ‘Dege
Eco Village' huko Kigamboni.
Akizungumza
wakati wa kukamilisha ziara yake
Kigamboni katika mradi wa nyumba
hizo, Pinda alisema Kigamboni inaendelea kwa kasi kubwa, kiasi kwamba
miundombinu iliyopo haitoshi kuhimili idadi ya watu watakaohamia.
“Tunahitaji
kujipanga kwa dhati kuhakikisha barabara na vivuko vinafanya kazi. Changamoto
kubwa hapa ni barabara za viungo kutoka Mandela upande wa Kurasini na upande wa
Kigamboni pia. Barabara hizi zote sita za darajani, zitatakiwa kufika
Kigamboni, Mjimwema, Mbagala na kwingineko,” alisema.
Pinda
alisema daraja litakapokamilika, watumiaji watatozwa tozo la barabara ili kuweza kulihudumia.
Alisema serikali inafikiria pia namna ya kuipanga Kigamboni ili iendane na
maendeleo yanayokuja.
Kuhusu
mradi huo wa Dege Eco Village wenye uwezo wa kuchukua nyumba za ghorofa zaidi
ya 7,000 na za kawaida 300, Waziri mkuu
alisema mradi huo utaleta msukumo mkubwa kwa maendeleo ya taifa.
Pinda
alifurahishwa na kitendo cha NSSF, kuwapa kipaumbele wanachama wake kupata
nyumba ambazo zimejengwa katika mradi wa mfuko huo uliopo Mtoni Kijichi.
Tayari
nyumba 85 zilizojengwa katika awamu ya kwanza, zimeshachukuliwa na wanachama.
Ujenzi wa nyumba hizo ulianza Novemba 2008 na kukamilika 2010.
Nyumba
215 zilizojengwa katika awamu ya pili,
zimeshachukuliwa na wanachama na wadau wengine. Kwa mujibu wa Meneja Miradi, John Msemo, zilianza
kujengwa mwaka 2011 na kumalizika mwaka jana, ikiwa ni awamu ya tatu.
Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhani Dau alisema miradi yao ilikuwa inapata changamoto
kubwa, hasa upande wa barabara.
“Tukimaliza
ujenzi wa daraja tunategemea barabara zote jijini ziwe zimeisha ili kupunguza
msongamano katika daraja. Itakuwa haina maana kumaliza daraja wakati maungio
hayajakamilika,” alisema.
Aliongeza
pia kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali katika kutekeleza wa miradi hiyo,
ikiwemo ya kutopata ardhi kutoka kwa wananchi kwa muda unaofaa, serikali
kuchelewa kutoa asilimia 40 ya sehemu yake katika mradi na pia masuala ya
kitaalamu katika ujenzi wa daraja.
No comments:
Post a Comment