Kesi inayowakabili vijana saba wanaojiita ‘watoto wa
mbwa’, imeahirishwa hadi Agosti 15 mwaka huu, kutokana na hakimu anayesikiliza
shauri hilo, kutokuwepo mahakamani.
Akiahirisha shauri hilo juzi, Hakimu wa Mahakama ya
Wilaya ya Ilala, Tharasira Kisoka alisema kesi hiyo itaanza kusikilizwa tarehe
hiyo, kwani Hakimu Wilberforce Luhwago ambaye anasikiliza shauri hilo, hayupo.
Kesi hiyo imefikia hatua ya kusikilizwa, kutokana na
upelelezi wa shauri hilo, kukamilika. Watu hao walirudishwa rumande kutokana na
shauri hilo halina dhamana.
Washitakiwa hao ni Sijah Abdallah (19), Sadick Chitemo
(25), Shaibu (30), Balozi Inasio
(19), Zagomba Kihongo (20), Isack Lukosi (17) na Hatibu Rajabu (24), wote
wakazi wa Kiwalani Dar es Salaam.
Watu hao walidaiwa kuwa Januari mosi mwaka huu, maeneo ya
Yombo Kiwalani wilayani Ilala, waliiba Sh 150,000 na simu ya mkononi aina ya Nokia, mali ya Suma Fungo.
Ilidaiwa kuwa kabla ya tukio hilo
walimpiga mlalamikaji kwa mapanga na visu ili kuchukua vitu hivyo.
No comments:
Post a Comment