ANAYESHIKILIA REKODI YA KUISHI MIAKA 60 BILA KUOGA SASA ATAFUTA MCHUMBA...

Amou Haji.
Ni bachela na anatafuta mchumba.
Lakini, kuweza kukidhi matakwa ya moyo wake, unatakiwa kukubaliana na aina yake ya maisha isiyobadilika.
Amou Haji hajawahi kuoga kwa miaka 60 sasa, sababu anaamini kuwa msafi kutamfanya augue, na chakula chake akipendacho ni nungunungu waliooza.
Mapumziko yake hupenda kukaa chini na kuvuta, kwa kutumia kipande cha bomba kilichojazwa kinyesi cha wanyama.
Haji, mwenye umri wa miaka 80, anasema alichagua aina hii ya maisha baada ya kupitia kumbukumbu mbaya zilizojaa hisia wakati wa ujana wake na tangu hapo - pengine katika namna isiyoshangaza - akawa ametengwa kiasi fulani.
Makazi yake yapo katika kijiji cha Dejgah kwenye jimbo la kusini mwa Fars nchini Iran ambako, wakati fulani, kundi la vijana wa kiume walijitolea kutaka kumwogesha - lakini kwa bahati akafanikiwa kutoroka.
Wakati wa usiku ama hulala kwenye shimo ardhini, ambalo ni tulivu kama kaburi, au nje kwenye pagale matofali ambalo wakazi wa eneo hilo walijenga kwa ajili yake.
Kwa suala la usafi, Haji pia hapendelei chakula kisafi na kinywaji. Hupendelea mno nyama iliyooza ya wanyama waliokufa na lita tano za maji kwa siku kutoka kwenye pipa chafu la mafuta.
Lakini hatudhani Haji hajichungi mwenyewe - pale anapotaka kujifurahisha hutumia vioo vya magari kwa ajili ya kujisafisha, imeripotiwa.
Na pale anapohitaji kunyoa nywele, huzichoma nywele zake zilizojisokota kwenye moto.
Kwa mavazi, huvaa matambara na, kwenye baridi, kofia ya chuma ya vitani kutokomeza kabisa ubaridi.
Rekodi ya mwisho ya mtu aliyekaa muda mrefu bila kuoga ilikuwa ikishikiliwa na mwanaume wa India mwenye miaka 66, Kailash Singh, ambaye alikuja kuoga baada ya zaidi miaka 38.
Haji anadai ameshaivunja rekodi hiyo.

No comments: