KUSHOTO: Gemma siku chache kabla ya kifo chake. KULIA: Gemma akiigiza katika EastEnders ambapo alicheza mfululizo wa matukio zaidi ya 30. |
Gemma McCluskie mwenye miaka 29 nyota wa zamani wa EastEanders, aliangukiwa kwa muathirika wa dwa za kulevya Tony kufuatia maji machafu yaliyokuwa yakitiririka kwenye nyumba ya mama yao.
Alimtaka Tony kuondoa maji machafu hayo na anadaiwa kujibu mapigo kwa kumuua na kumkatakata mwili wake kwa kutumia kisu kikubwa.
Mahakama ilielezwa mwanaume huyo mwenye miaka 35 alijaribu kuwapoteza maboya polisi kwa kutuma ujumbe wa maandishi wa bashashi kwenye simu ya mkononi ya dada yake huyo aliyekufa siku iliyofuata na kumalizia kwa maneno 'Nakupenda, xx'. Mabaki ya mwili wa Gemma yalipatikana siku tano baadaye.
Mahakama ya Old Bailey ilielezwa kwamba Gemma alimtuhumu kaka yake kwa kuiharibu nyumba ya mama yao, Pauline iliyoko Shoreditch, mashariki mwa London, wakati akiwa amelazwa hospitalini.
Pia alichoshwa na tabia ya kaka yake kutopea katika matumizi ya dawa za kulevya - akivuta hadi misokoto 20 ya bangi mfululizo - na kuwaeleza rafiki zake: "Ameganda kama jiwe milele. Kitu cha kwanza asubuhi anaweka msokoto wa bangi mdomoni na haelewi anachofanya."
Crispin Aylett QC, akiendesha mashitaka, alisema marafiki walisikia Gemma akizozana na kaka yake baada ya kufungulia koki ya maji bafuni kwao Machi 1, mwaka jana.
Walipoonda wameshindwa kumfikia wakaanza kumpigia simu na kumtumia meseji za mashaka lakini Tony aliwaachia 'mbio za bata bukini'.
Aliwatumia meseji moja ikisema: "Hakuchukua gari, funguo ziko kando ya jiko na hatuwezi kufahamu kama alichukua nguo zozote - anazo nyingi mno!"
Hatimaye Tony aliripoti kutoweka kwa dada yake lakini taarifa alizotoa polisi ziliwaongoza kumweka katika orodha 'yenye utata'.
Mamia ya marafiki walikaa kikao kwenye baa na kutoka kwenda kusambaza vipeperushi wakidai taarifa.
Siku tano baadaye tishari katika mfereji huko Regent, mjini Hackney liligonga sanduku lililokuwa likielea, ambalo lilipasuka na kubainisha mabaki hayo ya viungo vya binadamu.
Gemma alitambuliwa kwa mchoro mdogo kwenye kifundo katika mwili wake. Hadi usiku uliofuata, mikono yake na miguu ilipatikana ikiwa kivyake.
Lakini kichwa chake hakikupatikana hadi Septemba kwa juhudi za watu wa kujitolea waliposafisha mfereji huo. Tony alikamatwa baada ya wapelelezi kukuta damu ya Gemma bafuni na kisu kilichotapakaa damu kilichotelekezwa jikoni.
Damu pia ilikutwa kwenye gari yake ndogo aliyotumia. Dereva aliwaeleza polisi kwamba Tony alihangaika kushusha sanduku zito kutoka kwenye buti la gari kabla ya kulikokota kuelekea katika mfereji.
Aylett alisema: "Alifanya kila awezalo kujiondoa katika tuhuma. Kwa kufanya hivyo, alijibainisha mwenyewe kuwa ni mdanganyifu, mtu ambaye anaweza kuwahadaa polisi huku akidhani kwamba anaweza kuepuka jambo hili."
Alisema Tony mwanzoni alijifanya yuko tayari kutoa msaada katika kumtafuta dada yake na kushirikiana na polisi katika uchunguzi.
Aliwapa polisi jina la rafiki wa kiume wa zamani ambaye alimkopesha Gemma fedha na kumtaja mmiliki wa duka la kababu ambaye anadhani alimwona Gemma baada ya kutoweka kwake.
Alifikia pia kudai kuwa mama yake alimweleza kuwa alitembelewa na Gemma siku moja baada ya kuwa ameuawa.
Aylett alisema: "Kufikia hapo polisi hawakuwa na sababu ya kumshuku yeye kwamba anahusika.
"Kwa hakika alikuwa akiwaongoza polisi kwenye mbio za bata bukini kwamba alikuwa na hila zake.
Tony, mkazi wa Shoreditch, ametiwa hatiani kwa kusababisha kifo cha dada yake lakini amekana kuua.
Anadai kuwa aliondoka baada ya kuzozana na Gemma na kwamba hahusiki na kumuua, mahakama ilielezwa. Kesi inaendelea.
Gemma alikuwa na miaka 17 wakati aliposhinda nafasi mchezo wa kuigiza wa BBC akicheza kama Kerry Skinner, mpwa wa Ethel Skinner. Alicheza sehemu 34 kabla ya kuachana na EastEnders mwaka 2001.
Mtaalamu wa elimu ya magonjwa amegundua kwamba alifariki kutokana na kupigwa mara tatu kichwani.
No comments:
Post a Comment