Wanafunzi wa Shule ya Msingi Misunkumilo wilayani Nkasi wakiwa darasani. |
Rais Jakaya Kikwete amesema ifikapo 2015 hakutakuwa na uhaba wa walimu nchini na kuanzia mwaka 2020, shule za msingi zitaanza kufundishwa na walimu wenye elimu ya shahada, kutokana na idadi kubwa ya wahitimu wa fani hiyo, watakaokuwa kwenye soko la ajira.
Kikwete alisema, katika nchi zilizoendelea, kuanzia chekechea walimu wana kiwango cha elimu ya shahada ya chuo kikuu na akaeleza kuwa kwa jinsi hali ilivyo nchini, ni wazi kuwa kuanzia 2020, itafikia huko.
"Kwa sasa hivi tunajiuliza walimu tutapata wapi, lakini niwahakikishie kuwa ifikapo mwaka 2015 hatutakuwa na tatizo la walimu tena na hadi kufikia 2020 tutajiuliza walimu waliopo tuwapeleke wapi na sehemu ya kwenda itakuwa ni kwa shule za chini,” alisema Rais Kikwete, Dar es Salaam jana.
Alikuwa akifungua Kongamano linalohusu Masuala ya Uchumi na Maendeleo, ambalo limeandaliwa na Kigoda cha Mwalimu Nyerere kwa kushirikiana na Kitivo cha Uchumi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kongamano hilo linajadili namna ya kuendeleza rasilimali watu ili mchango wake uonekane katika uchumi wa nchi.
Tanzania kwa sasa baada ya kufungua kwa wingi shule za sekondari za kata, imejikuta ina uhaba mkubwa wa walimu, hali inayofanya shule hizo kuwa na idadi ndogo ya walimu na kusababisha wanafunzi washindwe kufundishwa baadhi ya masomo.
Licha ya kukabiliwa na uhaba wa walimu, shule hizo pia zinakabiliwa na uhaba wa maabara, nyumba za walimu pamoja na vifaa vya kufundishia.
Hali hiyo, imefanya wanafunzi wengi wanaofeli kutoka kwenye shule hizo na hivyo kuzua kelele kutoka kwa wananchi kuwa elimu inayotolewa kwenye shule hizo haina ubora wowote.
Lakini Rais Kikwete katika hotuba yake, alisema katika eneo la elimu licha ya kuwa kuna changamoto kadhaa; lakini Serikali imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo kutokana na kuongezeka kwa idadi wanafunzi wanaoandikishwa darasa la kwanza, wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu na vile vya ufundi.
Alisema kutokana na kuongezeka kwa shule nyingi za sekondari, Serikali imeamua kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosomea ualimu katika vyuo vikuu na kwa kushirikiana na vyuo vikuu binafsi, ana uhakika wahitimu wa fani hiyo watakuwa wengi ambao watatosheleza mahitaji ya nchi na hivyo kufanya baadhi yao wapelekwe shule za msingi kufundisha.
“Upungufu utabaki kwa walimu wa masomo ya sayansi tu na hili kama taifa ni lazima tutafute suluhisho," alisema Rais Kikwete, ambaye katika eneo hilo la elimu, alisema changamoto bado ziko kwenye uhaba wa nyumba za walimu, ujenzi wa maabara pamoja na vifaa vya kufundishia.
Kwa upande wa nyumba za walimu, alisema Serikali imedhamiria kutatua tatizo hilo na akasema nyumba nyingi za vijijini ambako kuna shule za kata nyingi ni za udongo na nyasi ambazo hazina hadhi ya mwalimu kukaa na kuandaa masomo hivyo ni lazima walimu wajengewe nyumba bora.
Kwa upande wa afya, Rais Kikwete alisema wanaendelea kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na masomo ya udaktari na uuguzi, kuhakikisha nchi inakuwa na wataalamu wengi wa fani hiyo ili kupunguza uwiano uliopo kwa sasa ambao daktari mmoja anahudumia wananchi wengi kuliko ilivyo katika nchi zingine.
"Kwa hili ni lazima tukimbie wakati wengine wanatembea, tuko nyuma sana na naamini Muhimbili wakikamilisha upanuzi wa chuo na vyuo vingine kama cha Dodoma, tutakuwa katika hatua nzuri," alisema.
Kuhusu kilimo, Rais Kikwete alionesha masikitiko yake kuwa licha ya kuwa sekta hiyo ndio imeajiri idadi kubwa ya Watanzania, lakini mchango wake katika Pato la Taifa ni mdogo na pia sekta hiyo ukuaji wake pia umekuwa ni mdogo ukilinganisha na sekta zingine.
Alisema hali hiyo ndio imefanya umaskini uendelee kuwa mkubwa kwa wananchi licha ya kuwa takwimu za ukuaji wa uchumi wa nchi ni nzuri ambazo kwa sasa zinaenda kwenye asilimia 7.
Rais Kiwete alisema kazi iliyopo kwa sasa ambayo wasomi wanatakiwa kutoa mapendekezo ni namna ya kuboresha kilimo ili kitoe mchango mzuri katika ukuaji wa uchumi wa taifa.
“Ndio maana tumeamua tujikite zaidi huko na tumekuja na mipango mbalimbali yote hii ni kukifanya kilimo kiwe cha kisasa zaidi, tumefanikiwa katika sekta zingine ni lazima pia kilimo tukikwamue," alisema Rais Kikwete katika mkutano huo ambao umewajumuisha wachumi mbalimbali wazalendo.
Wachumi hao wametakiwa kubuni mikakati ya kuendeleza raslimali watu ili kuongeza mchango katika ukuaji wa uchumi.
Rais alisema kwa kutambua umuhimu wa kilimo ndio maana Serikali imedhamiria kuimarisha utafiti kwa kutenga fedha za kutosha na kwa kuanzia mwaka huu ambapo imetengwa Sh bilioni 30.
Fedha hizo kwa mujibu wa Rais Kikwete ni kwa ajili ya utafiti mbalimbali pamoja na kuimarisha taasisi za utafiti ambazo alisema zilikuwa taabani kwa kuwa zilikuwa zinategemea zaidi fedha za kigeni.
Alisema kinachosikitisha, mbegu zinazotumika nchini asilimia 75 zinaagizwa nje ya nchi, jambo ambalo alisema linaweza kuchangia uzalishaji mdogo katika sekta ya kilimo kwani mbegu hizo wakati mwingine haziendani na udongo pamoja na hali ya hewa nchini.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala alisema chuo hicho kwa kutambua mchango wake katika nchi, wameamua kuanzisha makongamano hayo na watayafanya kila mwaka ili kutoa fursa ya wasomi na wachumi kutoa maoni yao namna ya kuboresha maendeleo ya nchi.
Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Delphin Rwegasira alisema hatua ya taasisi hiyo iliyo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inalenga kupata mawazo ya kuimarisha uchumi wa nchi; ndoto ambayo alikuwa nayo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Dk Hassan Mshindo wa Tume ya Sayansi na Teknolojia katika mada yake alisema kuna tafiti nyingi zimefanywa katika eneo la kilimo, lakini cha ajabu ambacho wachumi wanatakiwa kujiuliza ni kwa nini tafiti hizo hazijasaidia kuboresha kilimo hadi kuruhusu sekta hiyo iendelee kudidimia.
Alitoa takwimu mbalimbali zinazoonesha kuwa Tanzania ina wasomi wengi ambao wamekuwa wanajikita kwenye tafiti mbalimbali kwa kushirikiana na raia wa kigeni na akaeleza kuwa mchango huo wa wasomi unatakiwa uonekane katika juhudi za taifa za kuboresha uchumi wake.
Profesa Samuel Wangwe alisema kuna kazi ya kufanya kwa sasa ni kuboresha uchumi na akashauri kuwa ni lazima kuwa na mawasiliano kati ya taasisi za utafiti, Serikali na sekta binafsi.
Pia alisema kuna haja ya taasisi za utafiti zishirikiane katika tafiti kwa kuwa na agenda ya mambo ya kushughulika nayo kwa kuzingatia vipaumbele ya taifa.

No comments:
Post a Comment