Wamiliki wa malori wanaosafirisha mizigo ndani na nje ya nchi, wamelalamikia kukithiri kwa wizi wa shaba wanayoisafirisha kunakofanyika nchini.
Wameeleza kuwa wizi huo, umesababisha mapato kushuka kwa kati ya asilimia 30 hadi 40, na kama hatua za haraka hazitachukuliwa, hali itakuwa mbaya zaidi.
Wameishauri Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi hasa Jeshi la Polisi, pamoja na wamiliki hao kukutana na kuona jinsi watakomesha wizi huo ili usiendelee kuathiri mapato yao na ya Taifa.
Katika hafla yao ya kusherehekeea miaka 51 ya Uhuru na kuzungumzia masuala mbalimbali waliyokumbana nayo kwa mwaka huu, wamiliki wa malori hayo ya usafirishaji mizigo, waliitaka Serikali kuthamini mchango wao katika maendeleo ya nchi na kuondoa vikwazo vingi vinavyowakabili.
Akizungumzia wizi huo, mmoja wa wamiliki hao, Angelina Ngalula alisema kwamba umesababisha katika miezi ya karibuni mizigo kupungua kupitishwa katika Bandari ya Dar es Salaam na badala yake sasa watu wanapitisha mizigo hiyo katika bandari za Walvis Bay nchini Namibia na Beira katika Msumbiji.
“Kwa kweli hali ni ngumu, hili ni tatizo kubwa na linatuathiri sana. Wizi wa shaba umekithiri hapa kwetu na umesababisha gharama za usafirishaji kupanda kwa sababu baadhi ya kampuni sasa zimekodisha magari ya ulinzi ya kusindikiza mizigo kutoka mgodini Zambia na inalipa dola za Marekani mia sita (600).
“Kwa hiyo, hapa unaongeza gharama nyingine. Lakini pia wizi huu sasa ni aibu kwa nchi. Na mbaya zaidi unafanyika hapa hapa Dar es Salaam. Mzigo unaweza kutoka mgodini ukavuka mpakani Tunduma, lakini ukaibiwa ukifika Dar es Salaam,” alifafanua Ngalula ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Bravo Logistics.
Alisema wezi wa shaba hiyo wanafahamika, ingawa hakutaka kuwataja hadharani na kueleza kuwa wamiliki hao na Jeshi la Polisi, wanapaswa kukaa pamoja na kujadiliana kuhusu njia za kukomesha wizi huo ili usiendelee kuathiri uchumi, kwa sababu ya mizigo kutopitishwa katika Bandari ya Dar es Salaam.
“Polisi wakitaka nitawasaidia, kwa sababu mimi mzigo wangu uliwahi kuibiwa katika yadi yangu, nikapambana hadi ukarudishwa. Nawajua vizuri wanaojihusisha na wizi huo, niko tayari kushirikiana na polisi katika kukabiliana na wizi huu kwa sababu unatuathiri sana.
“Lakini pia napenda kumpongeza Kamanda wa Polisi Dar es Salaam (Suleiman Kova), amefanya kazi kubwa sana katika kukabiliana na wizi huu, lakini yeye ni kwa Dar es Salaam pekee, hawezi kufanya kazi za Morogoro, Tunduma na kwingineko, ndio maana tutataka yawe ni mapambano ya wengi,” aliongeza mwanamama huyo alipozungumza jana na gazeti hili.
Alisema mzigo wake ulikuwa na thamani ya Dola za Marekani 100,000 (zaidi ya Sh milioni 150) na kwamba kuendelea kukithiri kwa wizi huo, kutasababisha kupoteza mapato mengi na kuifanya Bandari ya Dar es Salaam ikose biashara nyingi, wakati biashara hiyo haikuwa na ushindani na bandari za Beira na Walvis Bay.
Alisema pia kumekuwapo na ucheleweshaji wa mizigo katika mipaka, ikiwamo Kasumbalesa ambako wanaweza kusubiri zaidi ya siku 30 na Nakonde ambako wanalazimika kulipa Dola 30 hadi 60 kwa siku kwa gari kusubiria hapo na pia gharama za maegesho.
Aliwashauri wamiliki wenzake kuungana na kuanzisha maegesho yao maalumu ili kuondoka na usumbufu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Hivi karibuni, kumekuwapo na matukio ya wizi wa shaba kuripotiwa katika vyombo vya habari nchini. Baadhi ya wafanyabiashara na watu kadhaa jijini Dar es Salaam walikamatwa na wanaendelea na kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakihusishwa na wizi wa shaba kutoka Zambia.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati maalumu ya wamiliki hao wa malori, Ibrahim Ismail wa Usangu Logistics Ltd, alisema mbali ya kusherehekea miaka 51 ya Uhuru, wanamaliza mwaka wakiwa wamepata matatizo mbalimbali na kuishauri Serikali kuona umuhimu wa sekta hiyo muhimu kwa uchumi.
Alitaja baadhi ya matatizo kuwa ni usumbufu bandarini, kwa kuchelewa kutoka kwa mizigo kwa sababu mbalimbali, ikiwamo madai ya mifumo kutofanya kazi vizuri; wizi; mgomo wa madereva; kupanda kwa bei ya mafuta na gharama za uendeshaji; kuchelewa mipakani na tatizo kubwa la usalama.
Aliitaka Serikali kuona umuhimu mkubwa wa kuisaidia sekta hiyo ya usafirishaji, kutokana na mchango wake mkubwa katika uchumi na maendeleo ya nchi.
“Sisi ni wadau wakubwa wa maendeleo nchini. Serikali inapaswa kutuheshimu na kushirikiana nasi. Serikali iheshimu mchango wetu mkubwa. Iangalie masuala haya yote na kutusaidia. Tunaumia sana,” alisema Ibrahim na kuongeza kuwa kinachohitajika zaidi ni umoja na uongozi imara.
Kwa upande wao, wafanyabiashara wengine wamiliki wa malori hayo, wakiwamo Davis Mosha wa Delina, Azim Dewji wa Simba Trailers, Joel Metta na wengine, walihimiza ushirikiano na kutaka kuwa na chama imara kitakachosimama kutetea maslahi ya wamiliki hao.
Azim mbali ya kuwafanananisha wamiliki wa malori sawa na ombaomba, kutokana na kutoa fedha tangu mzigo unapopakiwa hadi kwenda kupakuliwa, alisema ipo haja ya Serikali kusikia vilio vyao na kuona jinsi ya kuwasaidia wasafirishaji hao.
Kuhusu chama chao, TATOA walikubaliana kuwa wataendesha uchaguzi Januari mwakani. Walihimizana kwamba ni lazima wahakikishe wanachagua viongozi watakaoweza kukifanya chama hicho, kiwe imara na kisimamie vyema majukumu yao na kiheshimike.

No comments:
Post a Comment