CHEKA TARATIBU...

Malaika mtoa roho maarufu kama Izraeli siku moja kaingia katika nyumba ya jamaa ambaye alikuwa anatakiwa kufa kwa mujibu wa orodha. Baada ya kuelezea dhumuni la safari yake, Izraeli akakaribishwa kiti na kuomba apatiwe maji ya kunywa. Jamaa kwa ujanja wake akaona ndio nafasi pekee ya kukwepa kifo. Akamletea maji ya kunywa lakini badala yake akaweka dawa za kulevya ndani yake. Baada ya kunywa Izraeli akalala fofofo, ndipo jamaa akatumia mwanya huo kufanya marekebisho katika ile orodha. Alifuta jina lake pale juu na kuliweka chini kabisa. Mara Izraeli akaamka na kutoa shukrani zake. "Kwa ukarimu ulionifanyia, badala ya kumchukua mtu wa juu ya orodha sasa nitaanzia kutoka chini!" Kasheshe...

No comments: