Godbless Lema. |
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa Wilaya na Mkoa wa Arusha pamoja na wapinzani wa chama hicho, wameamua kusafiri leo kwenda Dar es Salaam, kusikiliza hukumu ya kesi ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Hukumu ya Lema ni miongoni mwa hukumu zitakazotolewa na Mahakama ya Rufaa kesho kwa mujibu ratiba ya kesi zitakazotolewa hukumu na mahakama hiyo ambayo gazeti hili lilisomewa mahakamani jana.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa alisema wameamua kusafiri ili kushuhudia mbivu na mbichi ya hukumu hiyo.
Alisema wapo tayari kwa hukumu yoyote na wamejiandaa kusuka au kunyoa na kuongeza kuwa amepokea taarifa ya wanachama zaidi ya 100 wanaotaka kwenda Dar es Salaam kusikiliza hukumu hiyo.
Golugwa alisema hukumu hiyo inasubiriwa kwa hamu na wanachama wengi wamejitolea magari yao na fedha za nauli kwenda kusikiliza hukumu ya aliyekuwa Mbunge wao.
“Watu wa Arusha bado wanampenda Mbunge wao, na tupo tayari kusuka au kunyoa na hata kama tukirudi katika uchaguzi uhakika wa ushindi upo tu, jimbo hili ni la Chadema na si la CCM,’’ alitamba.
Awali, hukumu hiyo ilitolewa mwanzoni mwa Aprili mwaka huu na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Katika hukumu hiyo, Lema aliondolewa katika nafasi yake ya ubunge, lakini alikata rufaa.
Katika rufaa hiyo, Lema kupitia kwa mawakili wake, Method Kimomogoro akisaidiana na Tundu Lissu waliwasilisha hoja 18 za kupinga hukumu hiyo iliyomng’oa madarakani.
Walidai kuwa hukumu iliyotolewa haikukidhi vigezo na ushahidi uliotolewa haukuthibitisha mashitaka bila kuacha shaka. Pia walidai kuwa Jaji aliegemea ushahidi ambao haukidhi viwango.
Wakili Lissu alidai kuwa hakuna sheria ya uchaguzi inayoeleza matusi na maneno ya udhalilishaji yanaweza kuwa sababu ya kutengua matokeo ya uchaguzi.
Alifafanua katika madai hayo kuwa, katika Maadili ya Uchaguzi ndiko wanakataza maneno ya ubaguzi, udhalilishaji, maneno ya kashfa na adhabu yake ni faini ya kuanzia Sh 50,000 hadi 150,000.
Lissu alidai Sheria ya Uchaguzi haielezi kama maneno ya ubaguzi ni kosa la jinai, lakini wameeleza kuwa mtu atakayevunja maadili, ataadhibiwa kulingana na adhabu iliyotolewa kulingana na kanuni za maadili.
Kwa upande wake, Wakili wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Vitalis Timon, alidai kuwa matusi, kejeli na kashfa hayawezi kumvua ubunge Lema kwani wabunge wenyewe walitunga sheria Namba Nane ya mwaka 1995 ikiruhusu matusi baada ya kuona awali kuwa walikuwa wakibanwa na Mahakama.
Aidha, Timon alidai kuwa waliofungua kesi hiyo hawakuwa na haki ya kisheria kwa kuwa wanaohusika wakati wa kampeni ni wagombea, vyama vya siasa, mawakala wa wagombea na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) na kwamba wapiga kura wanahusika kulalamikia hatua za usajili wa wapiga kura na wakati wa kupiga kura.
Alidai wapigakura hawawezi kupinga matokeo ya uchaguzi wakati yanayotokea katika kampeni hayawahusu na katika ushahidi, walalamikaji walidai walimshauri Batilda (Dk Buriani aliyekuwa mgombea wa CCM) kwa muda mrefu afike mahakamani, lakini alikataa ndipo wakaamua kwenda wao mahakamani.
Naye Wakili wa wajibu rufani, Alute Mughwai aliiomba Mahakama kutupilia mbali rufani hiyo kwa kuwa hoja zilizotolewa na upande wa Lema hazitoshelezi kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu.

No comments:
Post a Comment