HUU NDIO MSITU WA MAUTI KATIKA MLIMA FUJI...

Hakika haijaweza kufahamika mara moja kwanini wengi wamekuwa wakichagua kujiua kwenye msitu, japo imeelezwa kwamba watu wa mwanzo kujiua walivutiwa na mandhari ya eneo hilo.
Azusa Hayano amesomea na kuishi kwenye msitu huo kwa zaidi ya miaka 30. Lakini bado hajapata jibu la sababu ya mwenendo huo wa mauaji hayo.
Haya ni mazingira ya kazi yake, ambapo mara kwa mara amekuwa na kazi ngumu ya kuvumbua miili ya watu waliojiua ama kukutana na wengine ambao wameoza kabisa. Anakadiria kwamba yeye mwenyewe amevumbua miili zaidi ya 100 katika miaka 20 iliyopita.
Mwanajiografia huyo mwenye umri wa kati aliwachukua watengenezaji filamu kutoka Vice.com hadi katikati ya msitu eneo linalojulikana kama 'Jukai' -bahari ya miti- kuwashirikisha alichojifunza.
Hata hivyo Hayano hakuweza kutoa majibu ya ufasaha kuhusu kwanini watu wengi wanajiua kwenye msitu huyo wa Aokigahara, lakini alizama kwenye mazoea ya wengi wao kupenda kupotelea humo wakiwa na lengo la kutorejea tena.
Katika filamu yake fupi ameelezea watengenezaji sinema jinsi gani miili inayosalia kwenye miti inavyoweza kuashiria matatizo aliyopitia mtu huyo kabla ya kuchukua uamuzi wa kujiua, na wakati mwingine kubadili mioyo yao na kuchagua kuishi.
Filamu hiyo inaanzia kwenye gari lililotelekezwa mpakani mwa msitu huo, huku ramani ikiwa wazi kwenye kiti cha mbele. Hayano akiwaambia wapigapicha kuwa imekuwa hapo kwa miezi.
"Nafikiri mmiliki wa gari aliingia msituni kupitia hapa na hakurejea." amesema.
"Nahisi walikwenda msituni wakiwa na matatizo kichwani."
Hayano, pamoja na mazoea aliyonayo kuhusu kifo, ameonekana kuwa na hofu sana. Kazi yake imempa mtazamo wa kipekee juu ya wote wanaojiua.
Kwa mtazamo wake, matukio ya kujiua nchini Japan yamebadilika kwa miaka. Anasema, "Haiwezekani ukafa kishujaa kwa kujiua."
Fuatilia video hizi zifuatazo kujionea mwenyewe.

 



No comments: