Mlevi mmoja baada ya kupiga mitungi maeneo ya Afrika Sana akaamua kurudi zake nyumbani. Lakini alipoingia tu kwenye gari akagundua kitu. Moja kwa moja akapiga simu Kituo cha Polisi Mabatini akiwapa taarifa kwamba alipoegesha gari kuna vibaka wameingia na kuiba usukani, redio, dashbodi na gia. Wakati polisi wakijiandaa kuelekea eneo la tukio, mara simu ikaita tena na sauti ya yule mlevi ikasikika, "Ooh afande! Usijali bwana nilikosea nikakaa kiti cha nyuma." Ama kweli ulevi noma...
No comments:
Post a Comment