CHEKA TARATIBU...

Mlevi mmoja kaingia baa huku akilia. Kwa huruma kijana aliyekaa jirani na mlangoni akamfuata na kumuuliza kulikoni? Yule mlevi akajibu, “Nimefanya kitu kibaya sana. Saa chache zilizopita nimemuuza mke wangu kwa bia saba  maana nilikuwa na kiu sana.” Yule kijana kwa uchungu akasema, “Doh, inasikitisha sana kuona amekwenda na sasa unataka arudi tena kwako, au sivyo?” Yule mlevi akajibu huku akiendelea kulia, “Haswaaaa.” Kijana akaendelea, “Pole kwa kumuuza na sasa umegundua kuwa bado unampenda, au sio?” Hapo mlevi akamkatisha na kujibu haraka, “Ooh hapana. Nataka arudi sababu nasikia tena kiu ya bia!”

No comments: