CHEKA TARATIBU...

Jamaa mmoja kaingia kwenye kihoteli kinachouza baga. Kamwita mhudumu na kuagiza kiasi kinachotosheleza mlo wake wa mchana. Baada ya muda kidogo mhudumu akamletea oda yake na bila kupoteza muda jamaa akaanza kula. Punde akaona nywele kwenye ile baga. Akamwita mhudumu na kumfokea sana kisha akamtaka ampeleke kwa mpishi mkuu kuona kinachoendelea huko. Bila ubishi mhudumu akamchukua jamaa hadi jikoni. Kabla hajaongea chochote jamaa akamuona yule mpishi mkuu akiendelea kutengeneza baga kwa kuziweka kwenye kwapa lake kabla ya kuingiza jikoni. Jamaa akang'aka, "Siamini macho yangu!" Hapo hapo mhudumu  akamjibu, "Unashangaa hivyo, je ukiona anavyotengeneza donati?"

No comments: