WAAMBIE SIDANGANYIKI... DARAJA LA KIGAMBONI LIKO TANZANIA BHANA...

Daraja jipya la Kigamboni ambalo sasa litajulikana kama "Daraja la Nyerere" lililozinduliwa rasmi jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli, kama linavyoonekana pichani. Daraja hili ndilo kubwa na la kisasa zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki likiwa na urefu wa mita 680. Daraja hili lina barabara sita za kupita magari, tatu kila upande. Pia lina njia za waenda kwa miguu zenye upana wa mita 2.5 moja kila upande. Kuna taarifa zilizozagaa zenye kupotosha kwamba eti daraja hili liko katika nchi jirani ya Kenya. Ni uongo... Daraja hili lililobatizwa jina ya DARAJA LA NYERERE liko jijini Dar es Salaam katika wilaya mpya ya Kigamboni.


No comments: