Kampuni ya Reli
Tanzania (TRL) imesema ubovu wa treni inayotoa huduma ya usafiri wa abiria katika jiji la Dar es Salaam unatokana
na kuzeeka kwa injini jambo linalosababisha kuwepo kwa
matatizo mbalimbali kama kuzima.
Msemaji wa TRL,
Midladjy Maez alisema hayo ofisini kwake
wakati akizungumza na HabariLeo
kuhusu ubovu wa treni hiyo iliyozimika
ikitoa huduma na kusababisha usumbufu kwa abiria.
“Yapo mambo
mengi ambayo siwezi kuyasema…uzee umeongezeka kwa injini hizo haswa ukikumbuka
kuwa zilipoanza kazi hazikuwa mpya bali ni zilizoboreshwa …ilikuwa kama huduma
ya reli yaanza kwa spana mkononi,” alisema Maez.
Alisema kila wakati huduma hiyo imekuwa na matatizo
yaliyokuwa yakihitaji marekebisho ya kiufundi
lakini kimsingi zinahitajika injini mpya za kisasa na tayari maombi ya vifaa hivyo
yalishawasilishwa serikalini tangu wakati wa Waziri aliyekuwapo Dk
Harrison Mwakyembe.
No comments:
Post a Comment