Wakati Jeshi la Polisi likilaumiwa
kutokana na namna lilivyoshughulikia maandamano ya Chama cha Wananchi (CUF)
wiki iliyopita, Serikali imetahadharishwa kuwa makini na harakati za kisiasa
zinazotumia mbinu za kuchokoza Jeshi la Polisi na kuvunja sheria halali.
Wakizungumza na mwandishi wiki hii kuhusu
dhana ya udhaifu wa jeshi hilo, baadhi ya watu wakiwemo wasomi wameitaka
Serikali kuwa makini na kauli za wanasiasa, ambao wamewahi kushiriki au kutoa
matamko ya kihalifu na leo wanatuhumu jeshi hilo.
Baadhi ya matukio ya kihalifu yaliyotajwa
kufanywa katika mazingira ya siasa, tamko la maandamano na migomo isiyokoma,
bila kibali cha Polisi, lililotolewa hivi karibuni na Mwenyekiti mwenza wa
Ukawa, Freeman Mbowe na udhalilishwaji wa Mkuu wa Wilaya, wakati wa uchaguzi
mdogo wa Igunga uliokuwa na ushindani wa kisiasa mwanzoni mwa 2011.
Tahadhari hiyo imetolewa, wakati Serikali
ikielezea kuridhishwa na kazi ya kutunza
amani nchini inayofanywa na jeshi hilo, na kuagiza lijiandae na siasa za 2015;
siasa za kabla ya Kura ya Maoni ya kupata Katiba Mpya na za kabla ya Uchaguzi
Mkuu ujao.
Akitoa tamko kuhusu kudhibitiwa kwa
maandamano ya CUF wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias
Chikawe, akizungumzia hoja ya mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia
(NCCR-Mageuzi), kuhusu polisi walivyodhibiti maandamano ya CUF, alisema Profesa Ibrahimu Lipumba, ambaye pia
ni Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, alikaidi zuio la Jeshi la Polisi.
Akifafanua zaidi, Chikawe alisema Januari 26 mwaka huu, Jeshi
la Polisi lilipokea barua kutoka CUF, iliyokuwa ikitoa taarifa za kufanyika kwa
maandamano kwenye viwanja vya Zakhiem Mbagala, Dar es Salaam.
“Maandamano yalipangwa kuanzia Temeke kwenda Zakhiem… Jeshi la Polisi liliwaita viongozi wa CUF kwa mazungumzo. Walifanya mazungumzo na Jeshi la Polisi lililotoa tahadhari kadhaa kutokana na sababu za kiusalama,” alisema Chikawe.
“Maandamano yalipangwa kuanzia Temeke kwenda Zakhiem… Jeshi la Polisi liliwaita viongozi wa CUF kwa mazungumzo. Walifanya mazungumzo na Jeshi la Polisi lililotoa tahadhari kadhaa kutokana na sababu za kiusalama,” alisema Chikawe.
Pamoja na CUF kuonekana kama vile
walielewa tahadhari hiyo, Chikawe alisema walishangazwa kuona Profesa Lipumba
akikaidi zuio la Jeshi la Polisi na kuamrisha wananchi kuandamana kuelekea
Zakhiem.
“Jeshi la polisi linataka kila mtu kutii sheria bila shuruti, na mtu yeyote akishindwa kufanya hivyo, Jeshi la Polisi litamshughulikia mtu bila kujali umri, jinsia, wala madaraka yake,” alieleza Chikawe kuonesha namna Lipumba alivyokaidi amri ya Polisi katika harakati hizo hizo za siasa za ushindani.
“Jeshi la polisi linataka kila mtu kutii sheria bila shuruti, na mtu yeyote akishindwa kufanya hivyo, Jeshi la Polisi litamshughulikia mtu bila kujali umri, jinsia, wala madaraka yake,” alieleza Chikawe kuonesha namna Lipumba alivyokaidi amri ya Polisi katika harakati hizo hizo za siasa za ushindani.
Akizungumza na mwandishi jana, Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), katika masuala ya Utawala na Siasa, Dk
Benson Bana, alishangaa Bunge kutumia fedha za umma, kujadili tukio la kiongozi
mmoja katika jamii aliyevunja sheria.
“Tuna viongozi wengi kuanzia wa kiroho,
wa kiutamaduni na wa kisiasa, inakuwaje kiongozi mmoja wa kisiasa akivunja
sheria Bunge likae kujadili?” alihoji, akizungumzia mjadala wa Bunge kuhusu
kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Profesa Lipumba.
Aliwataka Watanzania kuwa macho na mbinu
zinazotumika za kuchokoza vyombo vya dola na kukumbusha kuwa kuna chama kimoja,
ambacho hakukitaja jina, lakini ni Chadema, kilichotoa tamko la kuhakikisha
nchi haitawaliki mara baada ya kushindwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita.
“Yapo matamko mengi tu, lipo hata la
Mbowe la maandamano na migomo isiyokoma na katika matamko yote hayo, sijasikia
siku hata moja vyama vya upinzani vikisema Jeshi la Polisi linafanya kazi
vizuri.
“Kama unajua siasa za Tanzania, suala la
kuchokozwa Polisi ni la kawaida lakini ni vyema vyombo vya habari vitusaidie,
Polisi si chombo cha siasa ni cha amri, hakipaswi kuchokozwa… sisi tunalala
usiku na kuamka salama dhamana ya usingizi wetu tunawapa wao,” alisema.
Akielezea namna wanasiasa wanavyopenda
kuchokoza Polisi na vyombo vingine vya dola, alitoa mfano wa baadhi ya
wanasiasa kusimamisha walinzi binafsi nyuma yao, wakati wakihutubia mikutano ya
hadhara.
“Umeona katika nchi gani mwanasiasa
anasimamisha mlinzi nyuma kama Rais, wanajifananisha na Rais? Hii ni hadaa,
hawa wamelewa madaraka ambayo hawana,” alisema na kusisitiza umuhimu wa jamii
kuelimishwa ili wanasiasa waache kupima nguvu na vyombo vya dola.
Moja ya matamko ya kuchokoza Polisi, ni
lililowahi kutolewa na Mbowe la kufanya maandamano na migomo isiyokoma nchi
nzima, mwishoni mwa mwaka jana wakati wa
Mkutano Mkuu wa Chadema.
Mbowe aliyekuwa akiomba kuchaguliwa
katika nafasi hiyo kwa mara ya tatu mfululizo, na hivyo kuvunja utamaduni wa
chama hicho wa tangu kilipoasisiwa, kwa
kiongozi kuongoza kwa muda usiozidi vipindi viwili vya miaka mitano,
alitoa tangazo hilo kushinikiza kuvunjwa Bunge Maalumu la Katiba.
“Natangaza azimio la Mkutano Mkuu ni
kushirikisha umma kwa maandamano na migomo kwa kibali cha polisi na bila
kibali...siko tayari kwa mazungumzo tena, nchi haiwezi kubadilika kwa
mazungumzo ambayo ni kuchezea fedha za umma.
“Najua watatumia nguvu na kututisha na
silaha za moto. Lakini sisi tutasonga mbele,” alisema na kutaka kuundwe mtandao
wa Chadema na wananchi kushirikiana na
Ukawa kila wilaya, kufanya maandamano na migomo hiyo.
Aidha, aliagiza wanasheria wote wa Ukawa wakutane na kuona uwezekano wa kufungua kesi dhidi ya wajumbe wa Bunge hilo, kuwashambulia kisiasa wajumbe ambao ni wabunge katika majimbo yao ili kuhakikisha hawarejei tena katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Wakati mbinu hiyo ya kisiasa ikijionesha hadharani, Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Aboud Mohammed, amelitaka Jeshi la Polisi nchini kujipanga kukabiliana
na vurugu za kisiasa za 2015.
Aidha, aliagiza wanasheria wote wa Ukawa wakutane na kuona uwezekano wa kufungua kesi dhidi ya wajumbe wa Bunge hilo, kuwashambulia kisiasa wajumbe ambao ni wabunge katika majimbo yao ili kuhakikisha hawarejei tena katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment