KMKM YAJIWEKA PABAYA KLABU BINGWA AFRIKA


Mabingwa watetezi wa Zanzibar, KMKM imeanza vibaya kampeni yake ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 mbele ya mabingwa wa Sudan, Al Hilal katika mpambano uliomalizika muda mfupi uliopita kwenye Uwanja wa Tahlil, nchini Sudan.

Katika mechi hiyo ilikuwa na kasi ya aina yake, mabao ya washindi yalipatikana katika kipindi cha kwanza na hivyo kuwafanya wenyeji kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao hayo mawili.
Bao la kwanza liliwekwa kimiani na beki wa KMKM akiwa katika harakati za kuokoa wakati akikabiliana na mshambuliaji wa Al Hilal huku kipa wake akiwa ametoka langoni.
Bao la pili liliwekwa kimiani muda mfupi baadaye kutokana na piga nikupige langoni mwa KMKM na hivyo wenyeji kutumia makosa ya mabeki kujichanganya.
Timu hizo zitarudiana baada ya wiki mbili katika pambano linalotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Amaan, mjini Unguja.

No comments: