Baada
ya wakazi wa Dar es Salaam na Bagamoyo kukaa bila maji takribani siku nane,
hatimaye baadhi ya maeneo yameanza kupata maji baada ya matengenezo yaliyokuwa
yanafanyika kukamilika.
Akizungumza
na mwandishi, Ofisa Habari wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini Dar es
Salaam (DAWASCO), Theresia Mlengu alisema maji hayo yalianza kutoka baada ya
taarifa iliyotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu Jackson Midala, Januari 29, mwaka
huu.
Alisema
baada ya Ofisa Mtendaji Mkuu huyo kutangaza kuwa marekebisho ya mtambo
yamekamilika na huduma ya maji itarejea kama kawaida, kwa bahati mbaya saa chache baada ya maji kuanza
kutoka eneo lililofanyiwa marekebisho
liliharibika tena.
Aliongeza
kuwa mafundi waliendelea na kazi ili
kuhakikisha huduma hiyo inarejea kwa haraka, hatimaye juzi walifanikiwa
kukamilisha kazi na kuanzia jana asubuhi baadhi ya maeneo yaliyopo karibu na
eneo ulipo mtambo huo yalianza kupata maji.
Alisema
kutokana na umbali wa kilometa 50 kutoka eneo ulipo mtambo huo wakazi waishio
katikati ya mji watalazimika kuwa na subira kwani itachukua hadi masaa sita
maji kufika katikati ya mji.
Alisema maeneo yaliyokuwa yameathirika na
tatizo hilo ni Tegeta, Bagamoyo, Boko, Bunju, Bahari Beach, Sinza, Kinondoni,
Sinza, Mwenge, Chuo Kikuu, Ununio, Masaki, Mwananyamala, Magomeni na Msasani. mi,
nafasi aliyoishika hadi mwaka huu.
No comments:
Post a Comment