Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limepata
wenyeviti wapya wawili wa Bunge
watakaosaidia na Spika na Naibu Spika kuongoza vikao vya Bunge ambao ni Mbunge
wa Viti Maalumu, Lediana Mng’ong’o (CCM) na Mbunge wa Viti Maalumu, Kidawa
Hamis Saleh (CCM).
Mng’ong’o anachukua nafasi ya
mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama (CCM) aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi na baadaye kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu na Bunge).
Huku Saleh akichukua nafasi ya
Mbunge wa Jimbo la Uzini, Mohammed Seif Khatib (CCM) kwa upande wa Zanzibar
aliyeacha uenyekiti kwa sababu ambazo hazijafahamika.
Spika wa Bunge, Anne Makinda
akihitimisha kikao cha Bunge juzi jioni, alisema kamati ya uongozi ilipendekeza
majina hayo mawili kuziba nafasi hiyo na kwa mujibu wa kanuni za bunge yakiwa
majina mawili ambayo yalipitishwa na wabunge wote.
No comments:
Post a Comment