Mkazi wa Tabata, Erasto Clement (22) amepandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na kukana mashitaka ya kubaka na kumpa
ujauzito mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye umri wa miaka 16.
Akisomewa maelezo ya awali jana, Wakili wa Serikali Felista
Mosha alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan kuwa katika tarehe
na mwezi usiofahamika, mwaka jana, Clement pamoja na mlalamikaji walidaiwa kuwa
wanafahamiana kwa muda mrefu.
Mosha alidai kuwa Septemba, 2013 mshitakiwa na mlalamikaji
walianza mahusiano ya kimapenzi na kumuingilia kimwili mlalamikaji huyo huku
akijua kufanya hivyo ni kinyume na sheria.
Pia alieleza kuwa mlalamikaji aliripoti taarifa hizo katika
kituo cha Polisi na kupewa PF3 kwa ajili ya kwenda hospitali.
Wakili Mosha alidai kuwa mlalamikaji alipofika hospitali
alipimwa na kukutwa na ujauzito wa miezi sita.
Mshitakiwa alikubali maelezo yake binafsi pia alikana
kufikishwa mahakamani hapo kusomewa mashitaka yanayomkabili.
Hata hivyo, upande wa Jamhuri ulidai kuwa utakuwa na
mashahidi wanne na kielelezo kimoja ambacho ni PF3.
Hakimu Hassan aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili Mosi mwaka
huu itakapoanza kusikilizwa.
**Picha ya Maktaba**
No comments:
Post a Comment