Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
(OUT), Profesa Tolly Mbwette amechaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Chuo Kikuu cha
Afrika (Pan African University).
Atakuwa madarakani kwa miaka mitatu kuanzia
juzi aliposhinda katika uchaguzi uliofanyika jijini hapa.
Aidha, Ekwabi Mujungu amechaguliwa kuwa Mjumbe
wa Bodi ya Umoja wa Afrika inayoshughulika na mapambano dhidi ya rushwa kwa
kipindi cha miaka miwili ijayo.
Uteuzi wao unatarajiwa kuthibitishwa na
Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) utakaofanyika kwa
siku mbili kuanzia leo jijini hapa.
Katika mkutano huo, Rais Jakaya Kikwete
anatarajiwa kuwa miongoni mwa marais na wakuu wa nchi watakaoshiriki.
Serikali kupitia Ubalozi wake wa Addis Ababa
chini ya Balozi Naimi Azizi, ulipiga kampeni kuhakikisha kuwa wagombea hao
wanashinda nafasi hizo.
No comments:
Post a Comment