POLISI YAZIMA JARIBIO LA UJAMBAZI DARAJANI ZANZIBAR

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi limezima jaribio la ujambazi katika mtaa wa Darajani ambapo imewashika majambazi wawili huku mmoja akifanikiwa kutoroka.
Kamanda wa Polisi mkoa huo, Mkadam Khamis Mkadam alithibitisha kutokezea kwa tukio hilo ambapo alisema ni mapema sana kutoa taarifa hizo.
Mashuhuda wa tukio hilo ambalo lilikusanya umati wa watu katika eneo hilo la kibiashara  walieleza waliliona gari iliyokuwa na majambazi hao aina ya Noah yenye namba za usajili T736 CGT ikiingia kwa kasi kuelekea Vikokotoni.
Mmoja kati ya mashuhuda hao, Isack Festo (36) alisema gari hiyo iliyokuwa ikiendeshwa kwa kasi kwenye msongamano wa watu lilimgonga dada mmoja na ukuta na kushindwa kuendelea na safari.
Aliongeza kuwa wafanyabiashara katika eneo hilo walihofia kuwa imebeba majambazi hasa baada ya kuiona silaha.
“Ndani ya Noah hiyo mlikuwa na watu watatu, lakini walikuwa na hofu wakiangaza huku na huku, hapo ndipo tuliposhituka na kubaini kuwa ni majambazi”, alisema Isack.
Naye Hassan Abdulla Hassan alisema gari hiyo ilipakia majambazi ilikuwa ikikimbia kwa kasi ilikuwaikijaribu kuwa kwepa polisi ambao walikuwa wakilifukuza.
Alisema haikuchukua muda polisi ambao walikuwa kwenye nguo za kiraia wakiwa na silaha walianza kurusha risasi hewani kuwataka majambazi hao wajisalimishe.
Hata hivyo, wananchi waliokuwa katika eneo hilo waliwahi kuwatoa nje ya gari lao na kuanza kuwapa vipigo vikali.
Polisi walifika na kuwaokoa wakiwa hali mbaya ambapo walipata kipigo hicho muda mfupi kutokana na watu wengi kujaa katika eneo hilo.
Polisi baada ya kufika waliwachukua majambazi wawili wakiwa hoi, huku ikisemekana jambazi mmoja alifanikiwa kutoroka.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa majambazi hao walikurupusha na polisi baada ya kudaiwa kufanya tukio la kupora fedha kituo cha mauzo ya vocha za simu katika eneo la Mnazimmoja.
Katika tukio hilo watu watatu walijeruhiwa kutokana na kugongwa na gari la majambazi hao ambapo Fatma Salum amevunjia mkono, huku mkaazi wa Kianga, Mtumwa Bakari naye akijeruhiwa kwa kukatika mguu na mkono. vipimo vya X-ray.

No comments: