Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS), jana imezindua rasmi usambazaji wa matokeo ya sensa
ya watu na makazi ya mwaka 2012 kimkoa na kuanza na Mkoa
wa Pwani.
Uzinduzi
huo uliambatana na semina kwa watendaji wa mkoa huo, uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwamtumu Mahiza.
Mkoa
huo umekuwa wa kwanza kusambaziwa matokeo hayo, ili waangalie takwimu za mkoa
huo zilivyo na kuzitumia kupanga miradi
ya maendeleo kwa wananchi.
Mahiza
(pichani) alisema NBS wameanza kusambaza matokeo ya sensa hiyo kwenye mkoa huo kwa
wakati, kwani hivi sasa wanajiandaa kupanga bajeti ya mkoa kwa mwaka ujao wa
fedha.
Alisema
matumizi ya takwimu halisi na bora ni jambo la msingi ambalo linapaswa kufuatwa
na watendaji kuanzia ngazi ya kijiji, ili kupanga miradi ya maendeleo kwa
makini kwa kuzingatia mahitaji ya maeneo husika.
"Tuwashukuru
NBS, wameanza hapa kwetu kusambaza matokeo ya sensa na hili limekuja kwa
wakati, tupo kwenye kuandaa bajeti ya mkoa wetu hivyo tutatumia matokeo ya
sensa hiyo kupanga bajeti yetu,"alisema Mahiza.
Aidha
alisema ni vyema watendaji kwenye ngazi mbalimbali kuanzia mkoa hadi kijiji
wakawafafanulia wananchi kwenye maeneo yao juu ya matokeo hayo, ili waangalie
jinsi ya kupanga miradi ya maendeleo kulingana na mahitaji ya eneo husika.
1 comment:
I truly love your site.. Very nice colors & theme. Did you create this website yourself?
Please reply back as I'm attempting to create my own website and would love to find out where you got this from or just what
the theme is called. Thanks!
Post a Comment