RAIS KIKWETE KUKUTANA NA WAJUMBE WA UKAWA

Vyama vyote vya siasa nchini vikiwemo vinavyounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vitakutana na Rais Jakaya Kikwete kabla ya mwisho wa wiki hii, kujadiliana na kushauriana juu ya maendeleo ya mchakato wa Katiba mpya.
Vyama hivyo vya siasa vitakutana na Rais kwa mwavuli waKituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na vitakutana siku yoyote kuanzia leo kabla ya mwisho wa wiki hii.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa juu ya kikao hicho cha kukutana na Rais Kikwete, Mwenyekiti wa TCD ambaye pia ni Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, amesema mkutano huo ni matokeo ya barua waliyomwandikia Rais.
Akifafanua, alisema viongozi wa vyama hivyo vya siasa walikubaliana kukutana na Rais Kikwete, ndipo walipomuandikia barua ya kumuomba akutane nao na Rais akawajibu kuwa atakutana nao kabla ya mwisho wa wiki hii.
Vyama hivyo vya siasa ni pamoja na vinavyounda Ukawa ambavyo ni CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi ambavyo viongozi wake wamethibitisha kushiriki kwenye mkutano na Rais Kikwete.
Vyama vingine vitakavyoshiriki ni CCM, TLP, UDP na UPDP inayowakilisha vyama visivyokuwa na wabunge.  Uamuzi wa kuomba kukutana na Rais Kikwete, ulipatikana baada ya viongozi wa vyama hivyo kuketi kwenye mkutano wa wakuu wa vyama Agosti 23 mwaka huu, kujadili na kutafakari maendeleo ya mchakato wa Katiba mpya.
Alipoulizwa Cheyo ni mara ngapi wamejaribu kukutana na RaisKikwete alisema: “Mimi nimeshangaa Rais kutukubalia kwani hii ni  mara ya kwanza kumuomba na yeye amekubali na kusema kabla ya mwisho wa wiki hii atakutana nasi.”
“Hii ilitokana na viongozi wa vyama vya siasa pamoja namambo mengine kuazimia kutafuta nafasi ya kuonana na Rais Kikwete kwa lengo la kushauriana naye na Mwenyekiti waTCD (Cheyo) niliwasiliana naye na kuomba nafasi ya wajumbe wa TCD kuonana naye,” alisema.
Mwandishi alipomtafuta Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, ambayeni sehemu ya Ukawa, James Mbatia, alithibitisha kuwa atashiriki kwenye kikao hicho na Rais Kikwete.
“Sisi tunakwenda kukutana na Rais (Kikwete) kama TCD nahiyo imetokana na azimio la 16 katika mkutano uliofanyika Februari 12 na 13 mwaka huu, ambapo tuliazimia kuwa TCD iendelee na maridhiano ili kupata Katiba bora”.

No comments: