MALARIA YAUA MHAMIAJI HARAMU WA ETHIOPIA

Mmoja wa raia wa Ethiopia waliokamatwa kwenye msitu wilayani Bagamoyo wakituhumiwa kuwa wahamiaji haramu na kulazwa hospitalini kutokana na matatizo ya afya, amefariki akipatiwa matibabu.
Dawita Alalo (25) ambaye alikuwa miongoni mwa wahamiaji haramu 11 waliolazwa kwenye kituo cha afya cha Chalinze, wilayani Bagamoyo,  alifariki juzi  kwa ugonjwa wa malaria.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Athuman Mwambalaswa alisema Alalo alikuwa miongoni mwa raia 48 wa nchi hiyo walioingia nchini isivyo halali.
Walikamatwa Agosti 22 mwaka huu  wakiwa kwenye msitu wa Kijiji cha Visakazi Ubena Zomozi tarafa ya Chalinze.

No comments: