KAMPUNI YAZIDI KUJITANUA AFRIKA MASHARIKI

Kampuni iliyoteuliwa kusambaza kinywaji cha Bavaria Afrika Mashariki, Jovet (Tanzania) Limited, imesema inaanza kujitanua kisoko nchini na Afrika Mashariki hivi karibuni.
Kiwanda hiki chenye umri wa zaidi ya 300, kinatarajiwa kuongeza wigo wake ili kujiongezea utambulisho zaidi kwenye soko katika bidhaa inazosambaza.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saalam katika hafla ya chakula cha jioni cha mawakala wakubwa, kitakachojulikana kama ‘Mbio za Kuelekea Juu’, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, John Kessy alisema soko la kinywaji hicho limekua, hivyo kuna haja ya kutanua soko. 
Alisema Bavaria ni kiwanda cha pili kwa ukubwa nchini Uholanzi. Alisema kampuni ya Jovet inaamini ubora ni nguzo ya ustawi wao na kwamba  siku zote wamekuwa wakiangalia fursa mbalimbali za kuboresha hali ya wateja wake. 
“Tunaamini nguzo yetu kuu ni kuwa na bidhaa bora sokoni  na sisi tunaahidi wateja wetu waendelee kufurahia kilicho bora siku zote, sekta ya vinywaji inatarajiwa kupata mapinduzi makubwa kufuatia utanuzi huu wa kibiashara, ” alisema Kessy. 
Alisema Bavaria inawalenga wateja wa umri tofauti, kwa kutengeneza vinywaji vya aina mbalimbali, vyenye kilevi na visivyo na kilevi na vinywaji vya kuongeza nguvu. 
“Bavaria imekuwa ikiwafurahisha wateja wake kwa kutengeneza vinywaji vyenye mvuto na ladha tofauti, hivi karibuni tu Bavaria ilizindua kinywaji cha bia ya shayiri chenye ladha ya kakao na kahawa katika soko la Afrika ya Mashariki katika juhudi ya kujitambulisha zaidi,” alisema.

No comments: