WANAOSOMEA UALIMU WAONYWA

Wanafunzi wanaotarajia kujiunga na mafunzo ya Stashahada ya Ualimu wa Shule ya Msingi (ODPE) na Sekondari, wamepewa angalizo juu ya utaratibu wa kuomba udahili,  wakisisitizwa vyuo haviruhusiwi kudahili moja kwa moja.
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk  Primus Nkwera alitoa angalizo hilo jana wakati akizungumzia juu ya kuanza kwa kozi ya Stashahada ya Ualimu wa Shule ya Msingi (ODPE), inatakayoanza mwaka huu katika vyuo teule vya majaribio kwa waliomaliza Kidato cha Nne.
Dk Nkwera alisema  vyuo kwa sasa, haviruhusiwi kudahili wanafunzi moja kwa moja kwa kuwa jukumu hilo ni la Baraza.  Maombi ya kujiunga na kozi hizo, yanaanza kupokewa kesho hadi Agosti 31, kabla ya masomo kuanza Oktoba mwaka huu.
Alitaka waombaji wote na vyuo, kuzingatia taratibu za uombaji na udahili zilizowekwa,  kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza, ikiwemo kutotambuliwa kwa wadahaliwa kwa kuwa.
Mafunzo yataendeshwa katika vyuo  vilivyoteuliwa na Baraza, ambavyo vitaendesha mafunzo chini ya uangalizi wa karibu wa Baraza hilo, Taasisi ya Elimu na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Akizungumzia Kozi ya Stashahada maalumu ya Ualimu wa Sekondari kwa waliomaliza kidato cha nne kwa masomo ya Hisabati na Sayansi,  alisema itakaendeshwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Dk. Nkwera alisema waombaji wote wanatakiwa kuzingatia utaratibu wa uombaji, ambao ni kupitia njia ya mtandao kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja. “Baraza halitamtambua mwombaji yeyote atakayeomba kinyume na utaratibu uliowekwa,” alisema.

No comments: