UTUMISHI KUWAINGIZA WATANZANIA HISTORIA YA MASHUJAA

Wananchi mkoani Mbeya wametakiwa kuingia katika historia ya mashujaa kwa kulitumikia taifa la Tanzania kiuadilifu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro wakati akizungumza na wakazi jijini Mbeya waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mashujaa zilizofanyika katika maeneo ya Mnara wa Mwenge jijini hapa.
Kandoro alisema uwepo wa siku ya kuwakumbuka mashujaa kunaikumbusha jamii kutambua kuwa kuna watu waliojitolea kumwaga damu yao kwa ajili ya taifa lao.
Alisema wakati umefika sasa kwa wanajamii kujiuliza kizazi kijacho kitawakumbuka kwa mazuri yapi waliyoyatenda kwa taifa lao huku wenzao wakiwakumbuka kwa kumwaga damu kutetea taifa hili.

No comments: